Wednesday, April 11, 2012

Kanumba kazikwa, mamia wazimia



Jeneza lenye mwili wa marehemu Kanumba



HATIMAYE muigizaji namba moja wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba amezikwa, imebaki historia.


Jiji la Dar es Salaam, jana lilizizima kwa saa kadhaa wakati wa mazishi na maziko ya kijana huyo ' Kanumba The Great' aliyeaga dunia usiku wa kumkia jumamosi nyumbani kwake, Sinza Vatican, Dar es Salaam.


Mwili wa Kanumba ulifikishwa katika viwanja vya Leaders ukiwa umebebwa na wasanii na kuwekwa katika jukwaa maalumu.


Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa hakushuhudia maziko kwa kuwa alishindwa kuvumilia kuoa jeneza la mwanawe likishushwa kaburini hivyo alilazimika kuondolewa makaburini hapo.


Wakati gari lililobeba mwili huo likitolewa viwanja vya Leaders, wananchi walilizingira na kuimba “Mshushe tumbebe!”


Kelele hizo hazikuzaa matunda, kwani walikuwapo askari waliosimamia na kulinda usalama wa taratibu zote za mazishi.


Wananchi waliofurika viwanja vya Leaders walilalamika kuzuiwa kutoa heshima za mwisho kwa Kanumba, na wakalaumu waandaaji kwa kuweka utaratibu mbaya.


Wananchi hao walisema, kutokana na wingi wa watu ulioonekakana tangu nyumbani kwa Kanumba, Sinza, wahusika walipaswa kuzingatia hilo, na wangeandaa utaratibu ili wananchi wamuage msanii huyo katika Uwanja wa Taifa tangu Jumatatu na jana.



Inadaiwa kuwa mamia ya watu walipoteza fahamu wakiwamo waigizaji Wema Sepetu na Irene Uwoya.

No comments:

Post a Comment