
Umati wa watu waliokuwa katika eneo hilo, waliokuwa jirani na hapo na waliokuwa wakimiminika kwenda Leaders umesababisha shughuli hiyo isifanyike.
Mwili wa Kanumba umeshatolewa viwanja vya Leaders, unapelekwa katika makaburi ya Kinondoni utakapozikwa.
Kulikuwa na purukashani kwenye viwanja vya Leaders wakati wa kuliweka jeneza hilo kwenye gari kwa kuwa waombolezaji walitaka kuliona na hata kuligusa jeneza lenye mwili wa msanii huyo maarufu aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 28.
Kanumba, aliaga dunia usiku wa kuamkia Aprili 7, nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment