ZIKIWA zimesalia siku tano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki, kampeni hizo zimeingia katika hatua mbaya ya mnyukano wa kuchafuana, kutishiana vifo, huku vitendo vya rushwa vikidaiwa kushamiri hasa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Waraka huo ambao umekuwa gumzo mjini Arusha, unadaiwa kuandikwa na wabunge walijipambanua kama wapambanaji wa ufisadi, wakidai kuwa ni chaguo la mafisadi.
Waraka huo ambao Tanzania Daima Jumatano lina nakala yake, umesambazwa katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Chini ya waraka huo, kuna picha za wabunge wa CCM, akiwemo Anne Kilango (Same Mashariki), Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC), Samwel Sitta, James Lembeli (Kahama), Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, na Mchungaji wa Kanisa la Uzima na Wokovu Kawe, Josephat Gwajima.
Waraka huo unadai kuwa kiongozi mmoja aliyejiuzulu kwa tuhuma ya ufisadi ambaye hakutajwa jina lake, ndiye aliyemwaga pesa jimboni humo kuhakikisha Sioi anapitishwa ndani ya vikao vya CCM kugombea ubunge wa jimbo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na marehemu Jeremia Sumari.
“Lengo la kigogo huyo ni kujitambulisha kama mwanasiasa mwenye nguvu zaidi kwa kutumia fedha zake. Alitumia mafedha mengi kumsaidia Sioi kuwabwaga wana CCM wenye maadili ya Kitanzania. Sote tulishuhudia umwagaji wa rushwa uliokithiri na hivyo kuwanyima kina Sarakikya (William) na Kaaya (Elirehema) haki yao,” inasomeka sehemu ya waraka huo.
Waraka huo wa ukurasa mmoja uliendelea kueleza kuwa wamekata tamaa na mafisadi huku wakiwashutumu kwa kumpa sumu iliyotengenezwa nchini Urusi, Dk. Mwakyembe na kumfanya ataabike kwa maumivu makali.
Waraka huo unadai kuwa Dk. Mwakyembe alipata sumu hiyo kutoka kwa kigogo huyo ambaye hakutajwa jina na badala yake ametajwa kwa sifa kuwa ni fisadi papa.
“Nasi wanachama wa CCM tunaochukia ufisadi na ufalme katika siasa za Tanzania tunawaomba enyi watu wa Arumeru mumtendee mwenzetu haki kwa kuhakikisha kuwa mgombea wa mafisadi kijana Sioi hapati kiti hicho cha ubunge. CCM hatutaki ubunge wa kurithishana.
Mbali ya hilo, mwelekeo wa kampeni hizo umebadilika baada ya jana kuwapo waraka mzito wa kumkataa mgombea wa CCM, Sioi Sumari.

Vivyo hivyo hatutaki kuwaona mafisadi wakiendelea kujiimarisha kwa ajili ya urais mwaka 2015,” ulisomeka waraka huo.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment