Kampuni inayojishughulisha na Huduma za Hoteli na Utalii Afrika Mashariki (Tourism Promotion Services (TPS) ambayo pia inamiliki hoteli za Serena imenunua hoteli ya Mövenpick Royal Palm ya jijni Dar es Salaam.
Hoteli hiyo sasa itabadilishwa jina na kuwa Dar es salaam Serena Hotel kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao.
TPS (D) Limited inamilikiwa na Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED), TPS Eastern Africa Limited (TPSEAL), PDM (Holdings) Limited, PROPARCO and NORFUND .
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSEAL, Mahmud Jan Mohamed katika taarifa yake kwa vyombo vya habari anasema,kufunguliwa kwa hoteli za Serena jijini Dar es Salaa ni utekelezaji wa mpango wa muda mrefu wa kufungua hoteli katika miji mikuu Afrika Mashariki, yaani “City Hotel Circuit”
Alisema kutokana na kuwapo kwa hoteli tanzu za Serena, hoteli hii itafaidika na mtandao ulioenea Tanzania, Zanzibar, Kenya, Msumbiji, Rwanda na Uganda. “ Lengo letu ni kupanua wigo wao nchini na maeneo mengine.
No comments:
Post a Comment