Thursday, November 3, 2011

'House girl' amfanyia kitu mbaya mtoto wa bosi wake

MTUMISHI wa ndani, Aziza Issa (20) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kumuingiza kitu kigumu kwenye sehemu zake za siri mtoto wa mwajiri wake.


Aziza alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi Joyce Minde.


Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, alidai kuwa Oktoba 29 mwaka huu katika eneo la Tabata Kisukuru, Aziza alimdhalilisha mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili na nusu kwa kumuingiza kitu hicho kigumu kwenye sehemu zake za siri.


Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa rumande hadi Novemba 16 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.


Katika hatua nyingine, Hassan Shaja alifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kuiba Sh milioni 2.9 katika ofisi za Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco).


Mwendesha Mashitaka Mkuu Naima Mwanga, alidai mbele ya Hakimu Karim Mushi kuwa usiku wa Oktoba 26 mwaka huu katika ofisi za Dawasco, Shaja aliiba fedha hizo. Alikana mashitaka.


Chanzo: Gazeti la HABARILEO

No comments:

Post a Comment