Wednesday, November 23, 2011

Breaking News- Lori la mafuta laangukia magari madogo

WATU kadhaa wanahofiwa kufa baada ya lori la mafuta aina ya Scania kuacha njia na kuyaangukia magari madogo katika barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam.


Lori hilo lilikuwa linatoka maeneo ya Ubungo, likaacha njia na kwenda upande wa pili wa barabara na kuyaangukia magari madogo yaliyokuwa yakitoka Buguruni kuelekea maeneo ya Ubungo.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, ajali hiyo imetokea muda mfupi uliopita, na hadi sasa lori hilo bado limeyafunika magari matatu.


Mmoja wa mashuhuda ameieleza blog hii kwamba, ameshuhudia mama mmoja aliyekufa, na kwamba kichwa kimetenganishwa na kiwiliwili.


Inadaiwa kuwa , hadi dakika chache zilizopita, mmoja wa watu waliokuwa kwenye moja ya magari hayo alikuwa bado kafunikwa na alikuwa ananyoosha mkono kuomba msaada.


Hadi sasa haijafahamika ni watu wangapi waliokuwa kwenye magari hayo ni na ni wangapi kati yao wamekufa.


Watu ni wengi eneo la tukio, wanajaribu kuwasaidia waliofunikwa lakini kutokana na uzito wa lori hilo ni wazi kuwa vinahitajika vyombo maalum ili kulitoa juu ya magari yaliyoangukiwa.

No comments:

Post a Comment