Michelle Obama ni mtetezi wa haki za wanawake, mdau wa maendeleo, na mpinga ubaguzi, awali alikuwa mke wa Seneta wa jimbo la Illinois, Obama na sasa ni First Lady wa taifa lenye nguvu kubwa kijeshi na kiuchumi.
Awali Michelle alipinga wazo la mumewe kugombea urais, hakutaka Obama awe miongoni mwa wagombea urais Marekani.
Obama alifanya kazi ya ziada kumshawishi Mwanasheria Michelle, akakubali na kushiriki kumuombea kura mumewe achaguliwe kuwaongoza Wamarekani.
Obama alikuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kugombea urais wa nchi hiyo, na akachaguliwa kumrithi George Walker Bush, na kuwa Rais wa 44 wa taifa hilo lenye uhusiano mzuri na Tanzania.
Januari 20, 2009 walihama Chicago na kuanza maisha mapya White House, Washington DC.
Jina kamili la Obama ni Barack "Barry" Hussein Obama, Jr, alizaliwa Agosti 4, 1961 Honolulu, Hawaii, alikulia huko huko Hawaii na Indonesia, baba yake mzazi ana asili ya Kenya. Jina kamili la mkewe ni Michelle LaVaughn Robinson, alizaliwa Januari 17, 1964 Chicago, Illinois.
Michelle ni mmoja wa watoto wawili wa Frasier na Marian Robinson, kaka yake, Craig (45) alitangulia kuzaliwa. Mwanamke huyo na kaka yake walikaa muda mrefu na mama yao kuliko baba yao.
Michelle alikuwa na uwezo mkubwa darasani na malengo, alipata nafasi ya kusoma katika shule ya watoto wenye vipaji maalum, alipotimiza umri wa miaka 13 alisoma somo la elimu ya viumbe.
Craig amesema, ingawa Michelle alikuwa mdogo kwake hakuwa mtu wa kumpuuza, na anakumbuka wakati fulani walikuwa wakicheza mchezo wa ‘ofisi’, walitengeneza vyumba viwili, yeye (Craig) alikuwa bosi, dada yake Katibu Muhtasi. Baba yao alifariki dunia mwaka 1990, mama yao yupo hai.

Barack Obama na Michelle siku ya ndoa yao.
Barack na Michelle walikutana mwaka 1989 katika mazingira ya kikazi, kwa mujibu wa mwanamke huyo, ‘alimdondokea’ Obama kwa sababu zinazofanana na zile zinazosababisha watu wengine wamheshimu mwanasiasa huyo, ni namna anavyounganika na watu.
Michelle amesema, Barack hakumuahidi maisha ya kitajiri, alimueleza kuwa wangeishi maisha mazuri, ametimiza ahadi. Mwanamke huyo yupo wazi, kwa nyakati tofauti amekuwa akisema kuwa alimpenda na anampenda Obama kwa sababu ana upendo, mvumilivu, na pia ana mvuto.
Michelle na ‘sweetheart’ wake walifahamiana wakati Barack alipokwenda kufanya mazoezi kwa vitendo ya taaluma sheria katika kampuni ya mawakili ya Sidley Austin iliyopo Chicago, Marekani wakati huo mwanamke huyo alikuwa ameajiriwa katika ofisi hiyo.
Wakati wakiendelea na kazi Obama ‘alimzimia’ Michelle akawa anatafuta nafasi ya ‘kumchombeza’, kwa nyakati tofauti akawa anamuomba watoke, kwa takribani mwezi mmoja mwanamke alikataa, baadaye Michelle alilegeza msimamo akakubali waende kula chakula cha usiku na baadaye waende kutazama sinema iitwayo Do the Right Thing.
Mambo yalizidi kunoga, wakafunga ndoa Oktoba 18, 1992, katika kanisa la Umoja wa Kristu la Trinity lililopo Chicago, Illinois.

Obama alipokwenda kumsalimu bibi yake nchini Kenya
Baada ya miaka saba walipata mtoto wa kwanza, Malia Ann Obama aliyezaliwa Julai 4,1998, mwaka 2001 wakajaliwa kupata mtoto wa pili Natasha “sasha”.
Kwa mujibu wa Michelle, mtoto wao wa kwanza, Malia anataka kuwa muigizaji, lakini kwanza anataka kusoma katika shule nzuri kama vile Yale ili akishindwa kuwa kuigiza apate kazi. Sasha yeye anapenda kuimba na kucheza, mama yao anawasaida wafahamu wanataka kufanya nini baadaye.
Amesema, ingawa Obama amekulia Hawaii, familia yake( ya Michelle) ilikuwa kama iliyomlea mwanasiasa huyo, Michelle kalelewa na bibi na babu kama Barack, na pia yeye alilelewa na mama mmoja kama Obama.

Michelle amesema, Barack Obama anayemfahamu leo ni sawa na yule ‘alimdondokea’ miaka ileeee.
Barack amesema Michelle ni mhimili wake, kitaaluma wanandoa hao ni wanasheria, walisoma chuo cha Harvard, wakati wanasoma hapo hawakuwa na uhusiano wa kimapenzi, Michelle alihitimu mwaka mmoja kabla ya Obama.
Kabla ya kusomea sheria na kutunukiwa shahada ya kwanza mwaka 1988 katika Chuo Kikuu cha Havard, Michelle alisoma masomo ya Sosholojia katika shule iliyopo Chuo Kikuu Princeton, alihitimu mwaka 1985.
Michelle amesema yeye na Obama wamepata malezi yanayofanana, wamefundishwa wafanye kazi kwa bidii ili wapate wanachotaka katika maisha yao, wafanye kile wanachokinena, na wathamini utu na heshima kwa watu wengine.
Michelle anasema, Barack Obama ni mwanaume mzuri, amejaliwa karama lakini ni mwanaume wa kawaida, na kwamba, mumewe ni ‘jibu’ kwa Marekani. Amesema yeye na mumewe wana imani na ndoto hali nzuri baadaye kama ilivyo kwa wamarekani wengine, na kwamba mumewe ni mchapa kazi na anaheshimu watu.
Amewahi pia kukaririwa akisema kuwa, Obama ana moyo wa aina yake na anafahamu sana masuala yanayowahusu wanawake yakiwamo matatizo yanayowakabili.
“Kwa kweli najaribu kuhakikisha watu wanamuelewa Barack ni nani kama mtu anayemuelewa vizuri zaidi, kuwafanya watu watuelewe” amesema na kueleza kuwa yeye na mumewe wana sifa nyingi za nje zinazofanana ikiwa ni pamoja na kupenda kukutana na watu na kujumuika nao.
Michelle ni mke wa mwanasiasa huyo mwenye asili ya Afrika, baba wa Barack ana asili ya Kenya, mama wa mwanasiasa huyo ni mmarekani wa Kansas, na kwa mujibu wa mke wa mgombea huyo, hisia za kumbagua mumewe hazina maana.
Obama amewahi kukaririwa akisema, ufahamu wake kuhusu uhusiano wa kimataifa hautokani na aliyofundishwa shuleni, anafahamu namna watu wa kipato cha chini kwenye nchi nyingine wanavyoishi.
Michelle ametoa mchango mkubwa kumpigia debe Obama lakini mara nyingi ushiriki wake umekuwa ukizingatia watoto wao wapo wapi,aidha shuleni, kambini au nyumbani na wanafanya nini.
Amekuwa akifanya safari za kisiasa kwa siku mbili tu kwa wiki na anapokwenda huko hakai hadi usiku labda akiwa na wanawe, asipoongozana nao hujitahidi kuwahi kurudi nyumbani ili awabusu kabla hawajalala. Michelle amesema mara nyingi hapati nafasi ya kupika ila ‘akiingia jikoni’ ni mpishi mzuri.
Baada ya Barack kuchaguliwa kuwa seneta waliamua kuendelea kuwalea watoto wao Chicago, Michelle akaendelea na kazi za taaluma yake. Mke wa mwanasiasa huyo amesema, uamuzi huo ulikuwa mzuri ili familia yao isitetereke. Watoto wao wanapata na malezi ya kiroho, kila jumapili familia hiyo huhuduria ibada katika Kanisa la Umoja wa Kristu la Trinity.
Pamoja na muonekano wa Michelle, sifa za kitaaluma, hulka yake na sifa nyinginezo katika jamii, ana sifa nyingine ambayo wengi hawaifahamu, anatajwa kuwa ni miongoni mwa wanawake wanaovaa vizuri zaidi, amewahi kuongoza katika orodha ya wanawake maarufu ‘wanaopiga pamba’ za nguvu.
Katika moja ya mikutano ya kampeni aliulizwa atafanya nini akifanikiwa kuwa First lady, alijibu kwamba atawalea wanae na kuhakikisha kwamba wanakuwa OK huko Ikulu, White House, sina hakika kama wataendelea na utaratibu wa familia yao kwenda Hawaii wakati wa sikuu za Christmas, dada na bibi mzaa mama wa Obama wanaishi huko.
Michelle amesema, kuna kazi inamsubiri na kama si hiyo atatafuta kitu kingine cha kufanya kwa kuwa hana wasiwasi kuhusu ajira kwa kuwa zipo tu, hivyo anawafikiria zaidi watoto wake anaowaita ‘my girls’. Alipohojiwa na jarida la New Yorker Michelle mwanasheria huyo alisema, kuwa mke wa mwanasiasa ni kazi ngumu na ndiyo maana Barack ni mwanaume mwenye shukurani.

No comments:
Post a Comment