SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imesema watu 197 wamekufa katika ajali ya mv Spice Islander iliyozama juzi Nungwi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kati ya watu hao 197 waliokufa, 158 wametambuliwa na kuzikwa na jamaa zao.

Kwa mujibu wa SMZ, marehemu wengine 39 hawakutambuliwa, Serikali imewazika kwa heshima zote katika eneo la Kama katika Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais Jakaya Kikwete ameagiza sayansi ya vinasaba (DNA), itumike mara moja kusaidia kazi ya utambuzi wa miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed amesema, watu 816 walionekana, 619 kati yao waliokolewa wakiwa hai, watu 319 walilazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi,baadaye waliruhusiwa wakabaki watu wanne tu.
Amesema, meli hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukua abiria 600 pamoja na tani 52 za mizigo, lakini kinachoonekana ilibeba mara mbili ya uwezo wake, kinyume cha abiria 610 waliokuwemo katika orodha halisi wakati meli ikiondoka Bandari ya Malindi.
Amesema, baadhi ya watu wanalalamika kutowaona jamaa zao waliosafiri katika meli hiyo na kusema kwamba upo uwezekano mkubwa wa baadhi ya maiti kuchukuliwa na maji kutokana na kasi ya maji katika eneo la mkondo wa Nungwi.
“Tumepokea malalamiko ya baadhi ya jamaa kusema kwamba hadi sasa hawajawaona ndugu zao ambao walisafiri katika chombo hicho. Upo wasiwasi mkubwa kwamba zipo maiti zimesombwa na maji na kupelekwa sehemu za mbali ikiwemo maeneo ya jirani kama Tanga
au Bagamoyo,” amesema.
Kuna taarifa zinazodai kwamba, kuna maiti zimeonekana mkoani Tanga.
Aboud ametaja chanzo cha ajali katika hatua za awali kama kuzidiwa kwa meli na wingi wa abiria pamoja na shehena ya mizigo.
Alipoulizwa kuhusu majaliwa ya nahodha na yupo wapi kwa sasa, alisema hajulikani alipo, limtaja kwa jina mmoja la Inyanyite.

Alisema inadaiwa wakati wa kizaazaa cha ajali, alisikika akisema atakufa na abiria katika meli hiyo. Kwa sasa wanamhoji mhandisi wa meli hiyo.
Aboud pia hakumtaja mmiliki halisi wa meli hiyo na kusema taarifa zaidi zitatolewa na bandari ambayo itakuwa inalifahamu suala hilo.

No comments:
Post a Comment