Monday, September 5, 2011

Joyce Kiria kaolewa tena

Mtangazaji wa kipindi cha televisheni cha Wanawake LIVE, Joyce Kiria jana alifunga ndoa na Henry John Kileo jijini Dar es Salaam.


Baada ya viapo maharusi na wageni waalikwa walikula 'bataz' Atrium Hotel, Afrika Sana - Sinza.


Desemba mwaka 2008, Joyce Kiria alifunga ndoa na DJ maarufu nchini, DJ Nelly au Nelson Joshua katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kijitonyama jijini Dar es Salaam.Wakati huyo Joyce alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Bongo Movies kilichokuwa kikirushwa na televisheni ya Channel Ten ya Dar es Salaam.


Juni 11 mwaka huu Joyce Kiria alijifungua mtoto wa kiume, amepewa jina Lincon Kileo

Picha zote kwa hisani ya blog ya Chini ya Carpet.

No comments:

Post a Comment