NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amekataa kutoa mwongozo kuhusu hoja ya Mbunge yeyote kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya 133 inayosema kwamba, Mbunge yeyote anaweza kupeleka hoja kwa maandishi kwa Spika wa Bunge kumweleza kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Ndugai alimruhusu Mnyika aisome kanuni hiyo mara mbili na akatoa uamuzi kuwa shughuli za Bunge ziendelee kwa kuwa kanuni hiyo inamtaka Mbunge awasilishe hoja hiyo kwa maandishi.
Kwa kuzingatia mantiki ya mwongozo aliouomba Mnyika, bila shaka, kama kanuni ingemruhusu atoe hoja hiyo bungeni, angetamka kuwa, hana imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa sababu ambazo angezitaja.
No comments:
Post a Comment