NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewaeleza wabunge kuwa, Mbunge anayetaka kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lazima awe amejiandaa vizuri kwa kuwa jambo hilo si dogo.
Kwa mujibu wa Ndugai, Mbunge akisema kuwa hana imani na Waziri Mkuu ina maana kuwa, HANA IMANI na SERIKALI hivyo ina maana serikali inapaswa kujiuzulu.
Ndugai amesema bungeni mjini Dodoma kuwa, Mbunge anaweza kutumia Kanuni za Bunge kuwasilisha hoja za kutokuwa na viongozi akiwemo Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Bunge na hata Rais wa Tanzania.
Amesema, Mbunge akiwasilisha hoja hiyo, Bunge litaipokea, lakini lazima iwe imewekwa saini na asilimia isiyopungua 20 ya wabunge wote.
Bunge la sasa lina wabunge 357, hivyo ili kuifikia asilimia hiyo, lazima wabunge wasiopungua 72 wawe wameweka saini.
Kwa mujibu wa Ndugai, Mbunge akitekeleza sharti hilo, wabunge wataijadili hoja yake, na watapiga kura za siri, na kwamba, matokeo ya kura utakuwa ndiyo uamuzi wa Bunge la Tanzania.
No comments:
Post a Comment