Monday, July 25, 2011

Changamoto kwa Serikali ya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda


Kuna mdau kanitumia hii,


Ili Serikali iweze kuongeza kima cha chini cha mishahara kwanza ipunguze posho na huduma za kulipia watumishi wa ngazi za juu mfano maji, umeme, simu ,nyumba na usafiri.


Wapo watumishi wana mishahara mikubwa halafu maji, umeme, nyumba, simu na usafiri wanalipiwaa na serikali lakini wenye mishahara midogo wanalipa wenyewe maji, simu, umeme, nyumba na usafiri.


Huu ni uonevu usiokubalika kwa nchi inayoongozwa na Serikali inayodai kuwa inajali usawa, inawathamini wanyonge na kupinga unyonyaji.


Na kama haitoshi, fedha wanazotoa wanyonge kulipia huduma hizo ndizo zinazotumika kuwalipa wakubwa posho za safari na vikao.


Hii inaonyesha kuwa pamoja na wakubwa kuwa na mishahara mikubwa bado watu wa mishahara midogo wanawachangia kwa kulipa maji, simu, nyumba, umeme na usafiri. Tafakari!

No comments:

Post a Comment