Thursday, May 12, 2011

Shabiki amshambulia kocha uwanjani

Kocha wa timu inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Scotland, Celtic, Neil Lennon (katikati)jana usiku alinusurika kupigwa makonde uwanjani wakati timu yake ikipambana na timu ya Hearts kwenye mpambano wa ligi inayoendelea nchini humo.

Shabiki anayeaminika kuwa ni wa timu ya Hearts (aliyevaa kofia) alimfuata kocha huyo mahali alipokuwa amesimama na kutaka kumpiga makonde lakini msaidizi wa Lennon, Alan Thompson(kushoto) alifanikuwa kuzuia mkono usimfikie mlengwa.

Mshambuliaji kakosa balance, konde linamkosa kocha (katikati), wanakuwa kama wanapishana



Shabiki alyetaka kumpiga kocha akiwa chini baada ya wanausalama kumzidi nguvu

No comments:

Post a Comment