Monday, May 2, 2011

Ni Osama kweli?





Televisheni nchini Pakistani imeonesha picha inayodaiwa kuwa ni ya maiti ya adui namba moja wa taifa la Marekani, Osama Bin Laden (54).


Rais Barack Obama ametangaza kuwa majeshi ya Marekani yamemuua Osama nyumbani kwake nchini Pakistan.



Inadaiwa kuwa, uchunguzi kwa kutumia vipimo vya DNA umefanywa kuthibitisha kuwa aliyeuawa ni Osama, na kwamba, mwili wake umeshazikwa.



Osama ametafutwa kwa zaidi ya miaka 10, na Marekani ilitangaza zawadi ya Dola milioni 25 kwa yeyote ambaye angekipata kichwa chake.

No comments:

Post a Comment