Wednesday, May 4, 2011

Mke wa Rais Obama anapojiachia

Si rahisi kumuona Mke wa Rais anacheza muziki au kuvaa mavazi unayoweza kusema kwamba anakwenda na fashion bila kujali umri wake, heshima yake katika jamii na pengine watu wanavyotarajia awe.



Mke wa Rais Barack Obama wa Marekani, Michelle Obama, yupo tofauti, anafanya yale anayojisikia na si kwa kutazama nani anamuangalia.



Leo ametembelea shule ya Harlem jijini New York nchini Marekani, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake kuhamasisha wanafunzi wafanye mazoezi ya viungo ili wasiwe tipwatipwa.


Ulipigwa wimbo wa Beyonce, mwanzo Michelle alijivunga kucheza, lakini akaona isiwe taabu, akajimwaga uwanjani, ilikuwa shangwe ile mbaya!

Sijawahi kumuona mke wa Rais yeyote yule anajiachia kama Michelle, big up mama!

Hapo , hapo , hapo , hapo!
Aah, raha sana



No comments:

Post a Comment