Tuesday, May 24, 2011

Mastaa na watoto wao

Beki mkongwe wa Man United, Rio Ferdinand akifurahia ubingwa akiwa na mwanawe, Lorenz

Mshambuliaji mkongwe wa Mashetani Wekundu, Ryan Giggs akiwa na mwanawe, Zach uwanjani Old Trafford mwishoni wa mwa wiki baada ya kukabidhiwa kombe la Ubingwa wa soka England.

Mshambuliaji nyota wa Man United, Wyne Rooney akiwa na mwanawe, Kai, wakati Man United wanashangilia ubingwa Old Trafford.

Man United wakishangilia ubingwa


Ni kawaida kuwaona mastaa wa Ulaya na Marekani wakiwa na wake zao, wachumba wao, na hata watoto wao lakini hapa Tanzania mmmhh!


Huenda si utamaduni wetu lakini siamini kwamba ni suala la mila na desturi kutofanya kama huko kwa wenzetu.


Kuna ubaya gani kwa mastaa wetu wa Bongo kuonekana na wenzi wao an watoto wao kama akina David Beckham, Brad Pit, Beyonce, Maria Carey, Anold Schwarznegger, Christiano Ronaldo n.k?


Lini Tutamuona Athumani Idd 'Chuji' , Masoud Kipanya, Asha Baraka, Phina Mango, Gaudence Mwaikimba, Haruna Moshi 'Boban', Juma Kaseja, Mrisho Ngassa, Ray, Kanumba, Mwana FA, A.Y, Mrisho Mpoto, Miriam Odemba, Ally Rwemtullah, Rose Mhando, Mwamvita Makamba, Aunt Ezekiel, n.k wakiwa na wenzi wao na watoto wao wakiwa huru bila hofu yeyote? Sehemu yoyote kama mastaa wa majuu?


Hivi kuna sababu za msingi kwa celebrities wa Tanzania kuwa wasiri kwa mambo kama haya?

No comments:

Post a Comment