Monday, May 16, 2011

Bosi IMF alisahau simu chumbani hotelini

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Dominique Sttauss-Kahn(62) akiwa chini ya ulinzi muda mfupi baada ya kushushwa kwenye ndege iliyokuwa inakwenda Ufaransa.


Mwanasiasa huyo anayetajia kugombea urais wa Ufaransa katika uchaguzi mkuu ujao, alitarajiwa kupandishwa kizimbani leo asubuhi mjini Manhattan kujibu mashitaka ya shambulizi na kujaribu kubaka.

Inadaiwa kuwa, bosi huyo wa IMF alimshika kwa nguvu na kutaka kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 32 aliyekuwa anafanya usafi katika chumba katika hoteli ya kifahari , Sofitel, nchini Marekani.


Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo, Mr Kahn alimvuta, akamlaza kitandani, alimvua suruali lakini hakufanikiwa kumbaka.


Inadaiwa kuwa, kabla ya jaribio hilo, bosi huyo wa IMF alitoka bafuni akiwa UCHI.


Kwa mujibu wa madai hayo, msichana aliyenusurika kubakwa alikimbia akaenda kutoa taarifa kwa viongozi wake hotelini hapo.


Muda mfupi baadae, katika kile kinachodhaniwa kuwa alikuwa anatoroka, bosi wa IMF aliondoka hotelini hapo, akasahau simu yake ya mkononi.


Muda mfupi baadaye, Mr Kahn alishushwa kwenye ndege iliyokuwa inajiandaa kuruka kwenda Ufaransa.


Bosi hiyo wa IMF hana kinga ya kidiplomasia hivyo akipatikana na hatia anaweza kufungwa jela miaka 15 hadi 20

Bosi wa IMF akiwa na mkewe, Mwandishi mwandamizi wa habari nchini Ufaransa, Anne Sinclair (63).

Mama huyo amesema, anaamini kuwa, mumewe hajafanya makosa anayodaiwa kuyafanya na atashinda kesi hiyo.


Hii ni mara ya pili kwa bosi huyo kupata misukosuko, mwaka 2008 alikumbwa na kashfa baada ya kubainika kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msaidizi wake IMF, akakiri na akaomba radhi.


Nyumba anayoishi Bosi wa IMF, jijini Washington D.C nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment