Monday, May 16, 2011

Alidhani mumewe mtulivu kumbe kicheche

Mke wa Kelvin anajivunia kuwa mumewe ni mtulivu, hashindi baa na hatongozi videmu!


Mama huyo anaamini kwamba, mumewe akitoka kazini huwa anakwenda kucheza basketball(mpira wa kikapu) na akitoka hapo anarudi nyumbani, wanakula pamoja chakula cha usiku (cha mezani).


Siku moja mama huyo akamhurumia mumewe, alimuona amechoka, akamshawishi watoke outing ili akapumzishe akili, arelax


Kelvin alikataa, kumbe mkewe alikuwa tayari amemuita dereva wa tax aje awachukue waende Gonga Club & Lodge.


Walipofika hapo wakakutana na mlinzi mlangoni, akasalimia , Mambo Kelvin! Kelvin akajibu "poa".


Mkewe akajiuliza inakuwaje mlinzi anakufahamu Kelvin?


Akamuuliza mumewe, akajibiwa kwamba yule Mgambo mchana analinda ofisini kwao (kwa akina Kelvin), usiku anapiga part time pale.


Wakaingia ndani, wakachagua meza, wakakaa, sekunde chache baadaye mhudumu akapeleka Castle Lager na kumuuliza yule mama anakunywa nini.


Mhudumu alipoondoka yule mama akamuuliza mumewe kwamba mhudumu amejuaje kwamba anakunywa Castle Lager, au wanafahamiana?.


Wakati Kelvin anafikiria ajibu nini, mhudumu wa vyumba akafika na kumweleza Kelvin kuwa, kama kawaida amemuandalia chumba namba tano, hivyo waingie tu vinywaji atawapelekea.


Yule mama alikasirika, akatukana, akaamkam akaondoka, akaenda nje na kukimbilia kwenye tax aliyoikuta nje.


Wakati anapatana bei na dereva, Kelvin naye akaingia kwenye gari hilo hilo, yule mama alikuwa bado anatukana kwa sauti huku anapiga kwikwi.


Dereva kuona vile, naye akasema, duh, eee bwana Kelvin huyu malaya uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa! Mamaa akazimiaaaa.

No comments:

Post a Comment