Monday, March 28, 2011

Mwanaume anataka nini kwa mwanamke?

KUNA mdau kanitumia hii, isome, bila shaka una jibu la hayo maswali aliyouliza.


Wanaume mnataka nini hasa kwa msichana, focus kubwa ya mwanaume kwa mwanamke ni nini? Sex, Feelings, Company au ni Nini?"


Ni nini Wanaume wanahitaji au wanataka kutoka kwa Mwanamke inatofautiana toka mwanaume na mwanaume na pia inategemea na mazingira yaliyowakutanisha.


Nimejaribu kufanya research ndogo. Source ya research yangu ni Mitandao na pia uelewa wa yale ambayo nimeyasikia toka kwa wanaume wengine.


Kwa kifupi haya ni baadhi ya mambo ambayo wanaume hasa walio juu ambao “any Woman would love to be with” au “Husband/Boyfriend Materials” wanahitaji:


1. Wanaume wote wameumbwa na ujasiri na wakati mwingine it is fun kwamba kuna baadhi ambao basi tu wanapenda kupata Mwanamke ambaye wanaamini kuwa ni mgumu kumpata.


Hapa nitatoa mfano ambao wakati niko chuo, ilimlazimu kijana moja ‘Mpenda Watoto” lakini ambaye kuna binti wa Kilokole alimkataa kwa ajili ya ukware wake; “Aokoke” naye na kutangaza ndoa na Yule binti ili mradi tu ampate.


Baada ya miezi 6 alifanikiwa na bila ya shaka hitaji lake lilikamilika.


2. Wanaume wanahitaji wanawake wenye afya njema: kimwili; kisaikolojia; kihisia na kifedha.


Wanawake wengi ni tegemezi katika mambo hayo na hili linawaweka katika nafasi mbaya mara mwanaume anapogundua kuwa huna vigezo hivyo. Wengi hawatakwambia ila wataishia tu.


3. Wanaume wanapenda wanawake wazuri kwa mwonekano” macho; mwili standard wa kibantu; nywele nzuri; mwili msafi ndani na nje na ngozi laini au nyororo isiyo na vipele au spots.


4. Wanaume wanataka wanawake ambao ni wakweli, wanaoweza kuaminika kwa kila wanaloongea liwe jema au baya.


Wanaume wengi wana multiple partners lakini hawategemei wanawake wanaowa-date wawe na partners wengine.


Kwa mfano, kuna vijana wana miaka 27 au 30 lakini akiwakusanya wanawake aliowachakachua wanajaa kwenye coaster, Marcopollo au DCM na wengine wanakosa seat, lakini wanaume wa msichana wake wanatosha kwenye Bajaj.


5. Wanaume wanataka wanawake wenye uelewa wa mambo mbalimbali. Ukiwa una interest zinazofanana na mwanaume basi ni positive point kwako.


Hakuna mwanaume anayependa kumdate mwanamke muda mrefu kama hata akimpeleka dinner hakuna maongezi.


6. Wanaume wanataka wanawake ambao watakuwa wanafanya effort ya vitendo ya kumfurahisha. Suprises za nguvu lakini bila kumgangamalia.


7. Wanaume wanataka Wanawake ambao kila wakati Wanaonekana maridhawa na wako smart na pia juu katika Mwonekano wao.


Hakuna Mwanaume smart hasa wa mjini atataka kudate binti ambaye ni outdated. Kumbuka sign nyingi zinazowavutia Wanaume ni Mwonekano wako.


8. Wanaume wanataka wanawake ambao wana PASSION ambayo itamfanya Mwanaume akutafute tena. So girls spoil your man ukipata nafasi hiyo.


9. Wanaume hawapendi wanawake wenye majidai na majigambo kuliko uhalisia wao.

No comments:

Post a Comment