Wednesday, January 19, 2011

Umewadanganya wangapi?

KUNA mdau kanitumia hii, isome, ni kweli?
Mapenzi ni kitu kisichodumu kwa muda mrefu (do not last longer or is something temporary).
Ni kwa sababu ya mapenzi (?) leo upo na uliyenaye na unajihisi ndiyo umefika.
Huenda baada ya muda utaachana na huyo na baada ya muda fulani utapata mwingine na utamsahau kabisa huyu uliyenaye sasa ambaye unahisi bila yeye dunia haikaliki.

Kuwa mweli katika nafsi yako, jiulize, tangu ulipoanza kuchakachua miaka ileeeh, ni wangapi umewaambia unawapenda kwa dhati lakini sasa haupo nao?
Umewadanganya wangapi kwa kuwatamkia maneno kama vile honey, sweetie, my love, baby, mahabuba, ma shababi, la aziz , nikinywa maji nakuona, sipati usingizi bila wewe, ukiniacha nitajiua n.k lakini leo yako wapi?

Kwa mtazamo wangu, mapenzi ni kama siasa (politics) zinazokaribiana na ukweli.
Licha ya kwamba binadamu anahitaji kupenda na kupendwa tusijisahau.

No comments:

Post a Comment