Tuesday, January 25, 2011

Chelsea: Man U tunakuja!

Mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba 'akifunguka' kupiga shuti lililotinga katika nyavu za Bolton. Kwa kweli hilo bao lilikuwa tamu na huenda litakuwa bao la msimu kama alivyosema yeye.
Mshambuliaji wa Chelsea, Malouda akifunga bao la pili.
Malouda akishangilia bao lake.
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia bao la nne lililofungwa na Ramires.
Raha ya bao la Ramires
'Mkoba' wa kutumainiwa wa Chelsea, John Terry, a.k.a Mwenye Timu, baada ya kumaliza shughuli ya kuwaua Bolton jana usiku kwa kuwatandika mabao 4-0.
Chelsea wanasema hawajawahi kukata tamaa ya kutetea taji lao la ubingwa wa England hivyo Man United wakae mkao wa kuliwa.

No comments:

Post a Comment