Zamani ilikuwa ni wanaume waliokuwa wakilalamika, kwamba wake zao hawataki kuwapa chakula cha usiku kama wanavyotaka lakini sasa ni zamu ya wanawake kulalamika.
Katika nyumba nyingi siku hizi hasa mijini wanawake ndiyo wanolalamika zaidi kukosa chakula cha usiku kwa waume zao.
Kwa nini?
Ukweli ni kwamba maisha yamebadilika sana,kila mtu anajitahidi sana kutaka kuhahakisha kwamba anafanya kazi hadi anaishiwa nguvu kabisa, akili na mwili vinachoka.
Wanaume wengi wanaolalamikiwa na wake zao kuhusu kupata uhaba wa chakula cha usiku ni wale wanaofanya kazi sana.
Ningependa kuwashauri wanaume kwamba wakati wanafanya kazi zao mchana wakumbuke kwamba kuna wake zao wapendwa ambao wanawasubiri jioni 'kuzungumza nao'.
Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake. Pamoja na kwamba ni muhimu kwao kufanya kazi, lakini wakumbuke kwamba kazi hazina mwisho.
Kuna jambo ambalo wanaume na hata wanawake hawalifahamu vizuri, hili ni lile linalohusu mazoezi.
Mtu anapofanya mazoezi anawezesha damu kuzunguka na kufikia sehemu zote za mwili kwa kiwango kinachotakiwa.
Kukaa ofisini kutwa na kurudi nyumbani na kukaa kwenye kochi na kuangalia TV siyo aina ya maisha inayoshauriwa tuishi.
Mwili unapochangamka kwa damu kufika kila mahali kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa chakula cha usiku na kukipokea huwa kubwa.
Lakini mbaya zaidi ni kwa wanawake wenyewe pia, wapo ambao bado wanaishi kwa miiko ya karne moja nyuma.
Hawa wanangoja wanaume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata mwaka watakaa wakilalamika kwamba hawapati chakula cha usiku.
Tukumbuke kwamba hata wanaume nao ni binadamu pia, huhitaji wakati mwingine kushtuliwa, wakishtua wao tu kila siku, kuna wakati hukinai.
No comments:
Post a Comment