Tuesday, March 31, 2009

Maswali ajali ya Chenge



KUNA mdau kanitumia huu ujumbe kuhusu ajali ya Chenge,

Kama bajaji zaweza kumaliza gari hivi basi bajaji zinatisha.Kwa upande wangu sikubaliani kwamba bajaji ina material ngumu kuweza kubonyeza gari hivi.

Labda kutokana na mtikisiko wa gari ilikwenda kugonga mti au kitu kingine chochote. Bajaji inaweza kweli kugonga gari na kuharibu hivi? Mimi nataka kujaribu kati ya tax na bajaji.

Hivi wanabidii hiyo ajali mnaielewa kweli?

Inasemekana Chenge alikuwa anatokea upande wa St. Peters kwenda Morogoro Store,Bajaji ilikuwa inatokea Morogoro Store, kwahiyo walikuwa wanakutana kwa usoni,Sasa iweje gari ya Chenge imebonyea upande wa kushoto na zaidi ya hiyo, iweje amemgonga kwa nyuma?

Na kwa material ya bajaj ni vigumu kuwa imesababisha madhara kama yale kwenye bodi ya gari
kama hilux afu kwenye boneti la gari ambako ni juu mno ya gari ukichukulia ukubwa wa bajaj,au
kuna gari la tatu ambalo halitajwi ktk tukio hili???????

Na kuna maelezo kuwa chenge alikuwa anfahamiana na mmoja wa marehemu na kwa mujibu wa mama wa marehemu, Chenge alikuwa akiwa mwanza hata kama Yule dada alikuwa off alikuwa anamuita [kumbuka dada alikuwa anafanya kazi mwanza hotel upande wa kasino]

Kama kuna mheshimiwa mjumbe ana majibu ya maswali haya tafadhali saidia

Ni kweli kuna limbwata?

KUNa mdau kanitumia ujumbe huu anaomba michango yenu

Nasikia kuna dawa ambayo wanawake wanawalisha waume zao kwa lengo la kuwatawala inaitwa Limbwata.

Nimeelezwa kwamba baada ya mwanaume kula limbwata anakuwa ZUZU, kila analoambiwa na mkewe anatekeleza, hivi ni kweli?

Naomba kufahamu kama ni kweli kuna dawa inaitwa limbwata au ni kitu cha kufikirika tu. kama kweli ipo ni dawa ya vidonge au maji? Mume akimpa mkewe inakuwaje?

Kuendesha gari lisilo na bima si kosa?



Chenge jana katika eneo la Mahakama ya Kindondoni, Dar es Salaam


KUNA utata kuhusu mashitaka yanayomkabili Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge baada ya kutoshitakiwa kwa kuendesha gari lisilo na bima.

Saa 10 usiku wa kuamkia Ijumaa gari alilokuwa akiendesha liligongana na Bajaj, watu wawili walikufa, Beatrice Costantine na Victoria George.

Jana alisomewa mashitaka matatu likiwamo la kuendesha gari kizembe, kusababisha vifo, na kusababisha uharibifu wa mali.


Saa chache baada ya ajali hiyo Chenge aliwaeleza polisi kuwa alikuwa akiendesha kwa speed kati ya 80 hadi 100.

Huko mitaani wananchi wamesikika wakiuliza, kwa nini hakushitakiwa pia kwa kuendesha gari lisilo na bima?

Monday, March 30, 2009

Chenge atapona?


MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge leo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Kinondoni kijibu tuhuma za kuhusika katika ajali iliyosababisha vifo vya watu wawili usiku wa kuamkia Ijumaa, Dar es Salaam.

Gari alilokuwa kiendesha aina ya Toyota Hilux liligongana na Bajaj Oysterbay, wanawake wawili wakazi wa Mwanza wakapoteza maisha.
Wanawake hao, Vicky Makanya na Beatrice Costantine walikuwa wanatoka kwenye ukumbi wa Starehe wa Club Maisha(zamani uliitwa Mambo Club) uliopo Oysterbay, Dar es Salaam.
Beatrice alikuwa anafanya biashara kati ya Mwanza na Zanzibar, ameacha watoto wanne, Scolastica, Daniel, Emanuel na Dereck, alizaa na mumewe, Stephen, wametengana.
Vicky alikuwa anafanya kazi Casino jijini Mwanza, Chenge amekaririwa akisema kuwa anamfahamu msichana huyo lakini amekanusha kuwa na uhusiano naye kuzidi ule wa kikazi.
Kwa mujibu wa kaka wa Beatrice, wasichana hao walifika Dar es Salaa Alhamisi, usiku wa siku hiyo hiyo wakafa ajalini.

Utata, nani baba wa mtoto Maisie?


Alfie, Chantelle na 'mtoto wao'

Maisie na 'baba'

'Baba na mwanae'


VIPIMO vya vinasaba(DNA) vimeonyesha kuwa yule mtoto mwenye umri wa miaka 13 aliyesema ni baba wa mtoto si baba wa mtoto huyo, Maisie.

Kabinti ka miaka 15, Chantelle Stedman aliutangazia umma kwamba Alfie ni baba mzazi wa Maisie kwa kuwa ni 'mwanaume' pekee aliyejamiiana nae.

Baada ya msichana huyo kusema hivyo walijitokeza wavulana kadhaa waliopinga kauli ya Chantelle kwa kudai kuwa mtoto huyo ni wao kwa kuwa wamehi kula uroda na mtoto huyo.
Alfie aliwaponda wavulana hao kusisitiza vichukuliwe vipimo vya DNA ili kuthibitisha kuwa yeye ni baba mzazi wa mtoto huyo.

Kitendawiliiii, tegaaa, nani baba wa Maisie?

Watoto wa Jade kutohudhuria mazishi


Jade, Jack, na watoto wa Jade, Freddie(Kushoto) na Bobby siku ya harusi Februari 22 mwaka huu

Jeff Braizer na Jade wakiwa na mtoto wao wa kwanza, Bobby

Jade akiwa na mwanae wa kwanza, Bobby baada ya kutoka katika jumba la Big Brother

Jade wakati akiumwa saratani ya kizazi

WATOTO wa Mtangazaji nyota wa vipindi halisi vya televisheni, Jade Goody(27) hawatahudhuria mazishi ya mama yao mzazi Jumamosi wiki hii.

Baba yao mzazi, Jeff Brazier(29) na bibi yao mzaa mama, Jackiey Budden(50) wameamua hivyo kwa maelezo kwamba Bobby(5) na Freddie(4) ni wadogo sana kuweza kustahimili kuona mama yao akizikwa.

Wamesema, kama watashuhudia mama yao akizikwa watabaki na kumbukumbu mbaya kuhusu mama yao hivyo hawatakwenda makaburini.
Jade alifariki dunia Machi 22 nyumbani kwake, aliugua saratani ya kizazi.

Waliokufa ajali ya treni Dodoma wangapi?







KUNA utata kuhusu idadi ya watu waliokufa katika ajali ya treni na gari moshi la mizigo iliyotokea usiku wa kuamkia jana wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Utata huo umesababishwa na taarifa za magazeti ya leo, kuna linalosema waliokufa ni 13, lingine linasema sita, lingine linasema wamekufa saba.

Ajali hiyo ilitokea saa 10 alfajiri Msagali katikati ya stesheni za Gulwe na Igandu

Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza iligonga kwa nyuma gari moshi la mizigo lililokuwa limesimama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa limeharibika.

tofauti ya idadi iliyotajwa katika magazeti inaashiria kwamba huenda idadi ya waliokufa ikawa kubwa zaidi ya 13 waliotajwa katika gazeti la leo kwa kuwa kuna abiria walikuwa wamebanwa katika mabehewa.

Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa ameagiza wakuu wa vituo vya Gulwe na Igandu wakamatwe wahojiwe na pia Kikosi cha polisi cha Reli kitoe taarida kuhusu ajali hiyo katika kipindi cha siku tatu kuanzia jana.

Ghorofa lanusurika kuungua Dar es Salaam

JENGO la ghorofa linalomilikiwa na Msajili wa Nyumba(NHC) kitalu namba 1285/84 jijini Dar es Salaam limenusurika kuungua usiku wa kuamkia leo.

Eneo la mgahawa katika jengo hilo Mtaa wa Zaramo imeungua, pembeni ya eneo sehemu hiyo kuna duka la nyama na chumba za biashara ya chips na kuku wa kupaka inayofanywa usiku.

Mashuhuda wamesema, moto huo ulizimwa kwa ushirikiano wa wananchi na magari ya zimamoto.

Sehemu ya juu ya jengo hilo linalotazamana na ofisi za DTV/ Channel Ten wanaishi wanafunzi wanaosoma katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Dalaam

Saturday, March 28, 2009

Polisi watuhumiwa kumuua dereva wa teksi


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

POLISI mkoani Dar es Salaam wanatuhumiwa kumuua dereva wa teksi kwa kumpiga risasi.

Inadaiwa kuwa polisi walimsimamisha dereva huyo aliyekuwa akiendesha teksi, alisimama, wakamuamuru afungue vioo alikataa, wakakivunja na kumpiga risasi akafa.

Mkuu wa Mkoa huo, Abbas Kandoro ameunda tume ya watu watano kuchunguza tukio hilo.

Kandoa amemtaja polisi aliyefyatua risasi hiyo kuwa ni, Koplo Aderbert Sangu, yupo polisi kwa tuhuma za mauaji.

Miaka michache iliyopita polisi mkoani humo waliwaua wafanyabiashara watatu wa madini na dereva wa teksi mmoja kwa tuhuma kwamba ni majambazi.

Rais Jakaya Kikwete aliuamuru iundwe tume kuchunguza ikabainika kwamba hawakuwa majambazi, kesi inaendelea Mahakama kuu Tanzania.

Friday, March 27, 2009

Masikini Chenge


Gari la Chenge baada ya ajali

Bajaj iliyogongwa


ALIYEKUWA Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge (61), leo aliwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, kwa zaidi ya saa saba baada ya kuhusishwa na ajali ya gari na Bajaj iliyoua watu wawili.

Waliokufa ni wanawake wawili ambao ndugu amejitokeza na kudai kuwa wote ni wageni waliwasili juzi Dar es Salaam kutoka Mwanza na mmoja alikuwa njiani kwenda Zanzibar kuolewa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ajali hiyo ilitokea saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia leo wakati Chenge akiendesha gari namba T 512 ACE aina ya Toyota Hilux na kuigonga Bajaj hiyo namba T 736 AXC iliyokuwa na dereva na abiria hao wawili wanawake.

Chanzo hicho kilidai kuwa baada ya ajali hiyo, Chenge alikwenda kwanza nyumbani kwake na kuwasili kituoni hapo saa moja asubuhi jana na kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa hadi saa saba mchana, huku nje akisubiriwa na ndugu zake.

Gazeti hili lilimshuhudia mbunge huyo wa Bariadi Magharibi akiingizwa kwenye gari la Polisi namba PT 0217 na kwenda eneo la tukio karibu na shule ya msingi ya Oysterbay katika makutano ya barabara za Karume na Haile Selassie, ambako alieleza namna ajali hiyo ilivyotokea.

Wakati mbunge huyo akitolewa katika kituo cha Polisi, kulitokea vurugu baina ya ndugu zake na waandishi wa habari, ndugu hao wakitaka kuzuia Chenge kupigwa picha, hali iliyosababisha kusukumana na kurushiana maneno makali.

Akiwa katika eneo la tukio, Chenge alimwelezea Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Peter Kivuyo, namna ajali hiyo ilivyotokea na alidai ilitokea baada ya Bajaj hiyo kutaka kupita gari lingine kwa kasi.

“Bajaj ile ilikuwa inataka kupita gari lingine lililokuwa likitoka Morogoro Stores, bahati mbaya kukawa na gari lingine linakuja, ile Bajaj ikabana upande wangu na mimi nilikuwa katika mwendo wa kati ya kilometa 80 hadi 100 kwa saa,“ alidai Chenge.

Alidai kuwa baada ya kuona bajaj ile inakwepa gari la mbele wasigongane uso kwa uso, alirudi upande wa kulia ndipo alipoigonga ubavuni kushoto. „Gari la nyuma lingesimama, dereva wake angeweza kueleza vizuri, ila baada ya ajali nikasikia watu wanaita ‚Chenge! Chenge!’ nikajua niko salama, nikashuka,“ alidai.

Aliendelea kudai kuwa aliposhuka, alikuta abiria wawili wanawake wakiwa bado wanapumua ingawa kwa shida, lakini walipofika Trafiki hali zao zilidi kuwa mbaya na katika kipindi hicho chote, dereva wa bajaj alikuwa haonekani.

Naye askari wa usalama barabarani aliyefika katika ajali hiyo, Mustafa Salum, alimweleza Kivuyo juu ya tukio hilo, ambapo alisema alipata taarifa za ajali hiyo saa 10.30 alfajiri na alipofika eneo la tukio, alikuta tayari abiria hao wawili wameshafariki dunia.

Naye kaka wa mmoja wa marehemu hao, January Constantine, alisema alipata taarifa za kifo cha dada yake, Beatrice Constantine (34), asubuhi na alikwenda kutambua mwili wake hospitalini, lakini kutokana na alivyopondeka alimtambua kwa alama za mwili.

Alisema dada yake ni mfanyabiashara na mkazi wa Mwanza na kwamba aliwasili Dar es Salaam, akiwa na rafiki yake huyo na ilikuwa aondoke jana alfajiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya harusi ya rafiki yake huyo.

Gari la Chenge kwa mbele lilikuwa na damu, nywele na mabaki ya ubongo ambao unasadikiwa kuwa wa mmoja wa marehemu hao. Polisi pia iliokota kipande cha fuvu la mtu katika eneo la tukio.

Gari hilo lilikuwa na stika ya Bima ambayo ilikatwa Juni 6, 2006 na kumaliza muda wake Juni 6, mwaka juzi.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mmiliki wa bajaj hiyo ni Zuwena Nassoro na anatakiwa kuripoti katika kituo chochote cha Polisi huku wakiwa wanamshikilia Chenge Oysterbay ili kuisaidia Polisi.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unafanywa chini ya Kivuyo na wataalamu mbalimbali ili kuondoa dhana ya upendeleo kwa kuwa Chenge ni mtu maarufu.

Chenge (62) alijiuzulu uwaziri wa miundombinu Aprili 20 mwaka jana, kutokana na kashfa ya rushwa ya dola milioni moja kutoka kampuni kubwa ya uuzaji vifaa vya kijeshi duniani ya BAE Systems.

Alijiuzulu baada ya kudaiwa kupokea rushwa ili kuwezesha ununuzi wa rada ya kijeshi ya pauni milioni 20 za Uingereza na kwamba fedha hizo ziliwekwa katika akaunti yake ya kisiwa cha Jersey.

Baada ya kujiuzulu, alikaririwa akisema pamoja na tuhuma hizo, mapenzi kwa nchi yake na chama chake, ndivyo vilimlazimisha achukue uamuzi huo na kuongeza kuwa fedha zilizokutwa katika akaunti yake hiyo hazina uhusiano wowote na BAE Systems.

Tuhuma hizo za rushwa zilichochea kelele pale alipohojiwa na waandishi wa habari na kujibu kuwa fedha anazotuhumiwa nazo ni 'vijisenti (fedha kidogo)'.

Rais Kikwete apangua wakuu wa wilaya

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya chini kwa kuwateua wapya 15, kuwastaafisha saba na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha pia kuwa Wakuu wa Wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Jumuiya za Chama Tawala.

Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa ni Bi. Mercy Silla (Arumeru, Arusha), Bw. Norman Sigalla (Hai, Kilimanjaro), Col. Issa E. Njiku (Misenyi, Kagera), Bi. Angelina Mabula (Karagwe, Kagera), Dkt. Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu, Manyara), Lt. Col. Benedict K. Kitenga (Rorya, Mara) na Lt. Col. Cosmas Kayombo (Mbarali, Mbeya).

Wengine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza); Bi. Queen Mwanshinga Mlozi (Ukerewe, Mwanza); Bi. Fatuma Mwassa (Mvomero, Morogoro); Bi. Fatma Ally (Nanyumbu, Mtwara); Bw. Juma Solomon Madaha (Tunduru, Ruvuma); Bw. Anatory Choya (Kishapu, Shinyanga) na Bw. Erasto Sima (Korogwe, Tanga).

Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa na vituo vyao kwenye mabano ni Bw. Elias Maarugu (Misenyi, Kagera); Bw. Deusdedit Mtambalike (Muleba, Kagera); Bw. David Holela (Babati, Manyara); Bi. Hawa Ngulume (Mbarali, Mbeya); Bw. Mashimba H. Mashimba (Kyela, Mbeya); Col. Peter Madaha (Nyamagana, Mwanza) na Bw. Gilbert Dololo (Kibaha , Pwani).

Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).

Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT.

Mtaani kwetu

Wingi wa masholi sio kipimo cha urijali

Mama wa Jade kuzibwa pengo


Jade alipokuwa mgonjwa

Mama mzazi wa Jade, Jackey Budden(50)

Mama mzazi wa Jade akitazama maua yaliyoachwa na waombolezaji

Mume wa Jade, Jack akiwavusha barabara watoto wa Jade

Mtoto wa kwanza wa Jade, Bobby(5)

Mtoto wa pili wa Jade, Freddie(4)

MMOJA wa washirika wa mtangazaji nyota wa vipindi halisi vya televisheni nchini Uingereza, Jade Goody amejitolea kuziba pengo la mama wa nyota huyo wa Big Brother kabla ya mazishi Aprili nne.

Jade alimuagiza mama yake mzazi, Jackiey asiende na pengo kumzika. Mtangazaji huyo aliyekuwa akisumbuliwa na saratani ya mfuko wa kizazi aliaga dunia Machi 22, ameach amume na watoto wawili.

Mtaalam wa masuala ya urembo, Nilam Patel amejitolea kuziba pengo hilo ili kutekeleza agizo la Jade.

Chenge atuhumiwa kuua kwa gari


MBUNGE wa Bariadi Mashariki mkoani Shinyanga, Andrew Chenge anadaiwa kujisalimisha polisi akituhumiwa kuua watu wawili katika ajali ya gari leo alfajiri.

Kuna madai kwamba Waziri huyo wa zamani amejisalimisha katika kituo cha polisi Oysterbay, Dar es Salaam, polisi wanatarajiwa kutoa taarifa zaidi baadaye.

kuna taarifa zinazodai kuwa mwansiasa huyo alikuwa akiendesha gari dogo lililogonga bajaj maeneo ya Oysterbay.

taarifa zaidi baadaye.

Thursday, March 26, 2009

Mrithi wa Amina Chifupa


MUDA si mrefu nimetoka ofisi za Clouds Entertainment Company Limited jengo la Kitega Uchumi Dar es Salaam kuzungumza na msichana anayewakuna wanawake wengi katika kipindi cha LEO TENA.
Kuna watu wanaomfahanisha na Amina Chifupa lakini anafahamu kuwa hawezi hata siku moja kufanana naye.
Uongozi wa Clouds FM umemkabidhi Dina Marius mikoba ya Chifupa tangu mwaka 2006 kuendesha kipindi hicho.
Kwa namna nilivyozungumza naye yupo tofauti na mtazamo wa wengi na hata yeye anafahamu kuwa watu wana mtazamo hasi kuhusu yeye wakiamini kuwa ni mbea, shangingi.
Mambo yote Jumapili kwenye HabariLEO Jumapili

Nyumbani kwa Sabato Masalia Dar es Salaam



Picha kwa hisani ya blog ya mzee wa Sumo
HIZO picha hapo juu ni makazi ya wanaodaiwa kuwa ni waumini wa dhehebu la Sabato Masalia walioweka kambi Tabata Dar es Salaam baada ya kutimuliwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini humo.
Wanasema wanasubiri kwenda ulaya kuhubiri Injili, hawana tiketi wala Visa!

Mume kuiomba msamaha maiti


Mume wa Jade Goody, Jack Tweed jana

Jade na Jack wakifunga ndoa Februari 22 mwaka huu

Jade na Jack walipokuwa boyfriend na girlfriend

Mama mzazi wa Jade akiwa na ua waliloacha mashabiki wa Jade nje ya nyumba yake(Jade)


MUME wa mtagazaji nyota wa vipindi halisi vya televisheni, Jade Goody(27) anapanga kwenda kuuona mwili wa marehemu mkewe ili amuombe msamaha na kumueleza kuwa anampenda.

Jack Tweed(21) anapanga kufanya hivyo kwa kuwa anajihisi ni mkosefu hivyo anapanga kutumias nafasi hiyo kumuomba Jade msmaha.

Jack amekuwa ni mtu wa majonzi tangu Jade afariki dunia Machi 22, na kila mara anabubujikwa na machozi.

Jack na Jade walifunga ndoa Februari 22, wamekuwa mke na mume kwa mwezi mmoja tu, na walilala pamoja usiku mmoja tu hotelini baada ya harusi yao.

Jade anatarajiwa kuzikwa Aprili nne, ameacha watoto wawili, Bobby(5) na Freddie(4)

Wednesday, March 25, 2009

Mtaani kwetu

"Aliyepewa kapewa, mpewa hapokonyeki"

Mshahara wa Mbunge milioni 7!?



Jengo la Bunge la Tanzania mjini Dodoma
SOMA nukuu hizi, duh, ebwana eeh

"Ndugu zangu afadhali msijue mshahara anaolipwa Dk Slaa kama Mbunge, mkijua nalipwa shilingi ngapi mnaweza hata kunipiga mawe"

"Mnataka kujua mshahara wangu, ninalipwa shilingi milioni saba kwa mwezi. Haki iko wapi? Mimi nalipwa shilingi milioni saba, na posho yangu kwa siku ni shilingi 135,000. Haya ni malipo makubwa mno, fedha ninayopata kwa siku inaweza kuzidi hata mshahara wa mwezi mzima wa polisi. Muulizeni yule polisi pale analipwa shilinig ngapi msikie"

"Juzi nimetaja posho za wabunge na kusema zipunguzwe, lakini Spika wa Bunge analalamika eti naingilia haki na madaraka ya Bunge, sasa leo nasema ninalipwa jumla ya shilingi milioni saba kwa mwezi, acha posho za bungeni. Kweli hii haki?"

Ni maneno ya Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa wakati akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Hedaru wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Dida wa Mchops atuhumiwa kusafirisha 'unga'

MTANGAZAJI wa Redio Times FM, inayomilikiwa na Kampuni ya Bussiness Times Ltd, Hadija Shaibu, maarufu kwa jina la ‘Dida wa Mchops’ anashikiliwa na askari wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi baada ya kumshuku kuwa anasafirisha dawa za kulevya.

Kuna madai kuwa Dida alikamatwa Juzi Jumatatu baada ya askari wa kitengo hicho waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kumkamata wakati akijiandaa kupanda ndege kwenda China.

Habari zilieleza kuwa Dida alikuwa akijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopian Airline, lakini polisi walilazimika kumtia nguvuni baada ya kumpeleleza kwa muda mrefu na kuhisi kuwa huenda siku hiyo alikuwa amemeza dawa hizo ili azisafirishe nje ya nchi.

Inadaiwa kuwa, baada ya Dida kukamatwa, alipelekwa kwenye choo maalumu kilichopo uwanjani hapo ambacho hutumiwa na askari wa kitengo hicho kuwahifadhi watuhumiwa wanaowakamata wakiwa wamemeza dawa za kulevya kwa muda ambapo endapo mtuhumiwa alikuwa amemeza dawa hizo atazitoa wakati akijisaidia.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa tangu alipoingizwa kwenye choo hicho juzi jioni hadi jana saa nne asubuhi, hakuweza kugundulika kuwa na dawa hizo tumboni ambapo alichukuliwa hadi makao Makuu ya Kitengo hicho, huko Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuhojiwa.

Taarifa zilizopo zinadai kuwa hajakutwa na pipi hata moja, na alidhaminiwa jana jioni.

Jade kuzikwa na gauni la harusi


Jade akiaga mashabiki wake wakati akitoka hotelini kurudi hospitali Februari 23 mwaka huu baada ya kufunga ndoa na Jack Tweed Februari 22.

Ilikuwa ni mara ya mwisho kwake kuonekana hadharani, alifariki dunia akiwa usingizini nyumbani kwake, Upshire, Essex nchini Uingereza.


Watoto wa Jade, Freddie(kushoto) na kaka yake, Bobby

Jade na Jack wakiapa kuwa mume na mke, Februari 22 mwaka huu.


Jade siku ya harusi yake Februari mwaka huu

NYOTA wa Big Brother Uingereza, Jade Goody atazikwa Aprili nne mwaka huu akiwa amevishwa gauni alilovaa siku alipofunga ndoa na Jack Tweed Februari 22 mwaka huu.

Kabla ya kuaga dunia Machi 22 mwaka huu, mtangazami huyo nyota kipindi halisi vya televisheni aliacha usia kwamba azikwe na gauni hilo na pete yake yake ya ndoa.

Jade pia alichagua picha ya wanawe, Bobby(5) na Freddie(4) hivyo itawekwa ndani ya jeneza lake.

Taarifa za kifo chake zimetawala vyombo vingi vya habar vya kimataifa na huenda mamilioni watashuhudia mazishi yake.

Tuesday, March 24, 2009

Wanafunzi kuwataja walimu wanaondekeza ngono

WANAFUNZI wa shule ya sekondari Lupanga mkoani Morogoro watapiga kura kuwataja walimu wanaoendekeza kufanya ngono na wanafunzi wa kike.

Wanafunzi hao wamegoma kuingia madarasani wakishinikiza walimu hao wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Watoto wa Jade wapo fit


Jeff akiwa watoto aliozaa na Jade

Bobby akifanya mazoezi baada ya kutoka shule jana

Freddie akitoka shule jana.

NYOTA wa shindano la Big Brother Uingereza, Jade Goody alikataa wanawe wasimuone dakika za mwisho wa uhai wake.
Jade aliitaka familia yake isiwapeleke wanawe, Bobby(5) na Freddie(4) alipokuwa akizidiwa kwa kuwa ingewaumiza.
Jade alizaa watoto hao na mtangazaji wa televisheni, Jeff aliyeishi nae kwa miaka mitatu. Huku akitambua kuwa siku zake za kuishi zilikuwa chache, Februari mwaka huu alifunga ndoa na akahakikisha wanawawe wanabatizwa.
Jumapili asubuhi Jeff alikuwa kazi ya ziada kuwaeleza wanawe kuwa mama yao ameaga dunia, alifanikiwa kufikisha ujumbe huo kwa kutumia picha ya ardhina mbingu.
Jade alifariki dunia Jumapili alfajiri kutokana na ugonjwa wa saratani ya kizazi iliyogundulika Agosti mwaka jana.

Monday, March 23, 2009

Gari lenye kura za Albino lashambuliwa

WATU wasiofahamika wamelishambulia gari la Halmashauri ya Wilaya ya Songea lililokuwa limebeba masanduku yenye kura za watuhumiwa wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, watuhumiwa wa ujambazi, wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya viungo vya binadamu na dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC), Ruvuma, kabla ya shambulizi hilo, kuna watu walipita mitaani kuwatangazia wananchi kuwa zoezi la kupiga kura hizo limesitishwa hivyo wasiende kupiga kura.

Kamanda wa polisi Ruvuma, Michael Kamuhanda amesema, polisi wanawasaka wahusika

Moto wateketeza hoteli mbili Bagamoyo


HOTELI mbili za kitalii wilayani Bagamoyo, Pwani zimeteketea kwa moto leo asubuhi.

Kwa mujibu wa polisi, moto huo umeteketeza Oceanic Bay Resort, na Paradise Beach Resort.

Moto huo ulianzia katika jiko la hoteli ya Paradise na ukasambaa hadi katika hoteli ya Oceanic.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Serengo mrengo sehemu kubwa ya mali za wateja zimeokolewa, ila mali za wamiliki nyingi zimeteketea.

Uongozi wa Hoteli ya Paradise umeahidi kuwa kesho utazungumza na waandishi wa habari ili kueleza kwa undani kuhusu ajali hiyo.

Raha ya kulea muulize mzazi



Huyo mtoto hata jina simfahamu, ila nilipenda kumbeba tulipokutana akiwa akiwa kabebwa na mama yake katika geti la kuingilia katika hifadhi ya taifa Mikumi mkoani Morogoro miezi kadhaa iliyopita.
Kuna mwenye swali?

Hoteli Bagamoyo zateketea kwa moto

HABARI nilizozipata hivi punde zinadai kuwa hoteli kadhaa katika ufukwe wa bahari ya Hindi wilayani Bagamoyo, Pwani zimeteketea kwa moto.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, moto bado unaendeelea kusambaa kwenye hoteli nyingine na juhudi za kuuzima zinaendelea.

Hoteli nyingi kwenye eneo hilo zimejengwa kwa makuti hivyo ni rahisi kushika moto.

Miaka michache iliyopita sehemu ya hoteli ya Sea Cliff, Dar es Salaam iliungua kwa moto.

Nyota Big Brother aaga dunia


Mwil wa jade ukitolewa nyumbani kweke kwenda kuhifadhiwa


Mama mzazi wa Jade, Jackiey wakati mwiili wa mwanae ukitolewa ndani kwenda kuhifadhiwa

Jade na tuzo yake

Jade baada ya madaktari kumueleza ana kansa ya kizazi

Jade akiaga mashabiki wake wakati akitoka hotelini baada ya kufunga ndoa Februari mwaka huu

Jade akiwa hospitali

Watoto wa Jade, Bobby(5) na Freddie(4)


NYOTA wa Big Brother na vipindi halisi vya televisheni Uingereza, Jade Goody(27) amefariki dunia akiwa usingizini nyumbani kwake, Upshire Essex nchini humo.

Bila shaka kifo hiki kimewasikitisha wengi nikiwamo mimi kutokana na yale aliyoyafanya katika siku za uhai wake.

Agosti mwaka jana madaktari waligundua kuwa, TV Star huyo alikuwa akisumbuliwa na kansa ya kizazi iliyosambaa kwenye sehemu nyingine za mwili.

Kabla ya kuaga dunia jana asubuhi, alikuwa akipoteza fahamu mara kwa mara na alikuwa kwenye maumivu makali.

Jade alifahamu kuwa hakuwa na siku nyingi za kuishi hivyo alifanya mambo kadhaa yatakayobaki katika kumbukumbu za wengi ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba na majarida na vituo vya televisheni ili apate fedha za kuwaachia wanawe, Bobby(5) na Freddie(4).

Watu wengi Uingereza, Ulaya na mabara mengine wamekuwa wakifuatilia taarifa za msichana huyo aliyepambana hadi dakika za mwisho.

Huku akiumwa na akifahamu kuwa ana asiku chache za kuishi, Februari 22 mwaka huu Jade alipanda madhabahuni kufunga ndoa na Jack Tweed, walilala pamoja usiku mmoja tu.

Alihakikisha kuwa kabla ya kuiaga dunia wanawe wanabatizwa, walipata huduma hiyo ya kiroho Machi saba mwaka huu, Machi 11 akajiruhusu kutoka hospitali akaenda nyumbani kwake kukisubiri kifo.

Mungu ailaze Roho ya Jade mahala pema peponi, amen.