Monday, September 14, 2009

Sala kabla ya tendo la ndoa


Jumuiya ya kanisa katoliki nchini Uingereza imewahimiza wanandoa wasali pamoja kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.
Jumuiya hiyo imetoa kitabu maalumu chenye mafundisho ya sala hizo zinazodaiwa kuwasaidia wasisikie maumivu wakati wa 'yale mambo yetu'.

Sala hiyo maalumu kwa ajili ya wanandoa imetolewa na kanisa katoliki nchini Uingereza ili kusafisha nia za wanandoa ili pia tendo la ndoa lisiwe na ubinafsi.

Kitabu chenye sala hiyo maalumu ambayo hufanyika kabla wanandoa hawajaanza kujamiiana ili kuwaondolea dhambi na kuwahamasisha wajitume 'wakati wa mchezo'

Kimeandaliwa maalumu kwa lengo la kuwafanya wanandoa wasafishike na madhambi ya kimwili wakati wa tendo hilo na wasifanye ubinafsi katika kutimiziana haja za kimwili.

Kitabu cha sala hizo kimechapishwa na Catholic Truth Society, jumuiya ya kanisa katoliki yenye makazi yake jijini London.

Kwa mujibu wa kitabu hicho, sala itakayofanywa na wanandoa kabla ya kujamiiana itawafanya wanandoa wajitolee kwa kila mmoja, mioyo yao kufunguka na upendo wa kweli kuongezeka.

Kitabu hicho,"Prayer Book for Spouses" kina sala mbali mbali maalumu kwa kila hatua ya ndoa na familia kuanzia hatua ya kuchumbiana mpaka kulea watoto.

Kitabu hicho kinasisitiza watu kufunga ndoa na kuishi pamoja milele huku kikilaani utoaji mimba.

Kitabu hicho chenye kurasa 64 kinawakosoa watu ambao wanaona ni vigumu kuishi na mtu mmoja milele, kipo madukani nchini Uingereza kinauzwa kwa paundi 1.95.

1 comment: