Wednesday, September 9, 2009

Mtoto wa mwaka mmoja ana mimba



Madaktari nchini China walipigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja ana mimba ya kichanga kingine.

Mtoto Kang Mengru wa nchini China alipelekwa hospitali baada ya wazazi wake kushtushwa na hali ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa siku hadi siku.

Baada ya mtoto huyo kufanyiwa ultrasound, madaktari waligundua kuwa mtoto huyo wa kike alikuwa amebeba kitoto kichanga kwenye tumbo lake ambacho kilikuwa kikiendelea kukua.

Madaktari wanaamini kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa na mimba ya watoto wawili mapacha na pacha mmoja alijitokeza ndani ya tumbo la pacha mwenzake.

Hali kama hiyo ya kichanga kuzaliwa ndani ya kichanga kingine ni nadra sana kutokea na humtokea mwanamke mmoja katika wanawake 500,000.

Mtoto Kang atafanyiwa upasuaji kukiondoa kichanga hicho tumboni mwake.

2 comments:

  1. oo my God!it cant be serious!May God be wit the child.

    ReplyDelete
  2. mh! jamani hivi ni kweli???
    mh! hiyo mimba imeingiaje jamani, au nayo ni mimba ya kichina??????wametuletea vitu vyao vya kichina, hadi mimba wanatuwekea

    ReplyDelete