Wednesday, September 2, 2009

Mama Zitto:Mwanangu si fisadi

MAMA mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto amesema, mwanae si fisadi na hanunuliki.

Amesema, viongozi katika makao makuu ya chama hicho ni 'wachafu', wanakiharibu chama.

Shida Salum amesema, Zitto hanunuliki na hawezi kununuliwa. Amesema jana Dar es Salaam kuwa, ofisi ya Makao Makuu ya Chadema itakiharibu chama hicho na anasikia aibu mwanae kutajwa kuwa ni mmoja wa mafisadi katika chama hicho.

Mwanachama huyo wa Chadema amesema, ofisi ya Makao Makuu Chadema imeingiliwa, na kwamba, chama hicho kimechafuka.

Salum ameyasema hayo mara baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kufungua mkutano wa uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA).

“Mimi fomu ya Zitto niliifukuza nyumbani kwangu, Zitto sio fisadi, hanunuliki na hawezi kununuliwa,” amesema mama Zitto.

Amesema,amekuwa katika chama hicho tangu mwaka 1992, na anasikia aibu sana zinapoibuka taarifa sasa kwamba mwanae ni miongoni mwa mafisadi.

No comments:

Post a Comment