MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana iliwaachia kwa dhamana viongozi wa wawili wa Taasisi ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (Deci) inayodaiwa jumla ya shilingi bilioni 39.27.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo,Jackson Mtaresi, Dominic Kigendi na Timothy Ole Loiting’inye juzi walitimiza masharti ya dhamana wakaachiwa hivyo washitakiwa wote katika kesi hiyo wameachiwa kwa dhamana.
Samwel Mtaresi na Arbogast Kipilimba juzi walirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Washitakiwa hao jana walitimiza masharti hayo ikiwa ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni 10 kila mmoja.
Mmoja kati ya wadhamini lazima awe mkazi wa Dar es salaam na anatakiwa aipe mahakama hati zake za kusafiria.
Mahakama imewaachia kwa kuwa Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) ametengua hati yake ya zuio la dhamana kuhusu washitakiwa hao.
Mahakama imewataka viongozi hao wa DECI wasifanye mkutano wowote unaohusiana na taasisi hiyo mpaka kesi itakapokwisha.
No comments:
Post a Comment