MADEREVA wa mabasi yanayokwenda mikoani kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo(UBT), Dar es Salaam WAMEGOMA.
Hadi saa mbili leo hakuna basi lolote lililotoka kituoni hapo kwenda mikoani.
Mamia ya abiria wapo wanasota kituoni hapo na hawana uhakika wa kusafiri leo.
Inadaiwa kwamba madereva hao wanapinga mwenzao kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuendesha basi kizembe na kusababisha ajali iliyoua na kujeruhi watu kadhaa.
Hata hivyo, kwa mujibu wa hukumu hiyo, ingawa dereva huyo kahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, adhabu za makosa yote zinakwenda pamoja hivyo atakaa jela miaka MITATU.
No comments:
Post a Comment