MABOMU yaliyolipuka Juzi Jumatano kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) yametekeza nyumba 50 na nyingine zimeharibika.
Mkuu wa kikosi cha anga JWTZ, Brigedia Jenerali Olomi amemweleza Rais Jakaya Kikwete kwamba, mabomu yalikuwa yanaruka, baadhi ya mabati katika nyumba za raia yametoka, na kuta zimeanguka.
Mabomu hayo yamesababisha familia nyingi kupoteza makazi na kutengana.
Wazazi wengi badi wanahaha kuwatafuta watoto wao, baadhi wametembea umbali mrefu na kwenda sehemu nyingi kuwatafuta.
Wananchi wengi hasa maeneo ya Mbagala hawana makazi, Serikali imewaambia wajiorodheshe hivyo huenda watalipwa fidia.
No comments:
Post a Comment