LEO ni siku ya mwisho ya mgomo wa wanawake wa Kenya waliokataa kufanya tendo la ndoa na waume wao na ma- single waligoma kufanya ngono ili kushinikiza wanasiasa nchini humo wamalize matatizo ya kisiasa.
Mgomo huo wa wiki moja ulianza Jumatano iliyopita, Mke wa Waziri Mkuu wa Kenya, Ida Odinga aliahidi kushiriki kwenye mgomo huo wa aina yake.
Kwa kuwa vitendo hivyo hufanywa kwa siri hakuna mwenye uhakika kama ni kweli waligoma na haieleweki wanaume walipokea vipi msimamo huo.
Kama ni kweli waligoma, huenda kuanzia kesho mambo yatakuwa shwari.
No comments:
Post a Comment