Sunday, May 3, 2009

Tanga si mchezo

NIPO mjini Tanga tangu jana, mambo shwari.
Tanga mchana kwa kiasi fulani inafanana na Zanzibar lakini usiku duh, ebwana eeh, yap yap yap!
Jana usiku mimi na wenzangu tulikwenda kuona live band ya Tanga, ilikuwa saafi sana.
Jamaa wanazipatia kweli nyimbo zamani, kuna mzee yaani anaziimba utadhani kazitunga yeye.
Leo mchana tulikwenda kwenye kituo kinachowatunza wasiojiweza kilichopo nje kidogo ya mji wa Tanga, kuna mambo nimeona yamenisikitisha.
Pale kituoni kuna mtoto anatambaa,mguu mmoja umefungwa POP nadhani umevunjika.
Nilimuona mzee anatembea kwa makalio, kweli tukiwa na viungo vyote na tukiwa wazima tumshukuru Mungu.
Jumapili njema.

No comments:

Post a Comment