Thursday, May 7, 2009

Mashabiki Uingereza watishia kumuua refa

POLISI nchini Uingereza leo asubuhi wamemtorosha refa aliyechezesha mpambano wa Chelsea na Barcelona baada ya muamuzi huyo, Tom Henning Ovrebo kutishiwa kuuawa.
Wachezaji wa Chelsea akiwa Didier drogba, Michael Ballack na John Terry jana walimzonga muamuzi huyo kwa wakimshutumu kuwa aliwanyima penati kadhaa.
Mlinzi wa timu hiyo, Bozingwa amesema, refa huyo ALINUNULIWA.
Andres Iniesta wa Barcelona alifunga bao katika dakika ya 93 lililowanyong'onyesha matajiri wa LONDON na kuzima ndoto za kucheza fainali za klabu bingwa Ulaya Mei 27 nchini Italia.

No comments:

Post a Comment