Tuesday, May 12, 2009

Mwanasoka kuoa 'mapema' faida au hasara?

Kiungo mshambuliaji wa AC Milan, Ricardo Kaka na mkewe, Caroline wakifurahi kupata mtoto, Luca Celico Leite aliyezaliwa Juni mwaka jana. Kaka kazaliwa mwaka 1982, alioa mwaka 2005

Mrisho Ngasa na mkewe, Latifa.
HIVI karibuni mshambuliaji wa klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam na timu ya taifa (Taifa Stars) Mrisho Ngasa alifunga ndoa na bibie Latifa.
Nimemuuliza mwandishi mwandamizi wa michezo kasema Ngasa ana umri wa miaka 21, lakini kuna sehemu nimesoma wanasema ana miaka 19
Wakati naperuuz kwenye blog ya Mzee wa Sumo nimekuta comments hizo hapo chini kuhusu ndoa ya mwanasoka huyo anayewania kucheza soka nje ya Tanzania.
Baadhi wametoa mtazamo wao kwa kumlinganisha na Wyne Rooney (Kaoa aanasubiri mtoto), Theo Walcot( hajaoa ila ana mchumba), Shown Write Philips (Hajao ila ana mtoto) Christian Ronaldo(hajaoa) nk.
Sijaongeza wala kupunguza neno kwenye comments hizo
Anonymous said...


Kwani ukiambiwa wachezaji wa Tanzania kwa nini hawawezi kuendelea utashangaa nn wakati sababu zinajulikana?,utajiri wetu ni ngono au kuoa,na hyo dogo hawezi kama mwendo wenyewe ndio huu.Anakimbilia nn jamani hajapata ushauri nn,hv anadhani christiani ronaldo,ronaldhino,kaka wameoa?hawana haraka maana kipindi cha kucheza mpira ni miaka 17 mpka 30 kama una uwezo sana mpka 35 sasa yeye anawahi nn wkt hata 25 hajafikisha?Hv hana mtu wa kumshauri?

Anonymous said...


Mwacheni bwana kila mtu duniani ana mipango yake, after all life expectancy ya bongo inaendelea kushuka, ngojeni kijana aonje kila analoweza kabla umri wa kufa haujafika, na pia tukumbuke mambo hayo husababishwa na mazingira ya mtu anayoishi na aliyokulia

Anonymous said...


kwani ngasa ana umri gani mpaka mseme kawahi kuoa?..na huyo mtoa maoni hapo juu anaesema angesubiri mpaka 35 ndio aoe..aache unafiki,afahamu kuwa ngasa akiwa kwenye ndoa ndio ataweza kutimiza malengo yake kwa sababu kwanza atakuwa hafanyi uzinzi na kubadilisha wanawake....
kama kwisha kwa viwango vya mpira basi wachezaji wa england wote wangekuwa na viwango duni kwani wanakuwa na wapenzi toka wakiwa under age...


walcott ana mpenzi wake,rooney ameoa ana miaka 22 na anatarajia kupata mtoto,shaun philips ana girlfriend na ana mtoto,nikiwaorodhesha wote hapa hapatotosha...hivyo jambo alilofanya ngasa hajakosea kabisa,


tatizo letu wabongo ni kula kulala mpaka katika age ambayo inabidi uwe na maisha yako,hivyo ukiona mtu katika age ndogo tayari kishafanya mambo ya maana basi mnajifanya washauri nasaha kwa kuleta fitina zenu....mwacheni ngasa ale bata..!

Anonymous said...


kwani kuoa na kucheza mpira wapi na wapi mbona ulaya wanaoa wakiwa wadogo na hatusemi kitu wacha unafiki kwenye mipingo ya mtu na kwa taharifa yako kaka anao watotowawili kwa huyu awala wake Ronaldo cha ngono sana hapo Man U mbona hushuke kiwango mpaka analala na ma-sister sita usiku mmoja ndoo hayo mnayataka afanye.shauri jambo baya lakini kuoa jambo zuri kabisa cha msingi aendeleee na mazoezi kama kawa ni hayo tu wadau.

Anonymous said...


kwani kuoa na kucheza mpira wapi na wapi mbona ulaya wanaoa wakiwa wadogo na hatusemi kitu wacha unafiki kwenye mipingo ya mtu na kwa taharifa yako kaka anao watotowawili kwa huyu awala wake Ronaldo cha ngono sana hapo man u mbona hushuke kiwango mpaka analala na ma-sister sita usiku mmoja ndoo hayo mnayataka afanye.shauri jambo baya lakini kuoa jambo zuri kabisa cha msingi aendeleee na mazoezi kama kawa ni hayo tu wadau.

CHIBIRITI. said...


Hongereni sana Ngasa & Latifa, ndo mtatulia vizuri na maisha.Na kuoa sio mwisho wa kucheza mpira kabisa, Ulaya wachezaji wengi sana wadogowadogo wameoa, kwasababu kuoa ni uwezo wa mtu na nimipango ya mtu, sasa kama maisha yapo fiti kwanini asioe? Hongera sana Ngasa usisikilize maneno yasio kuwa na mpango, jitahidi kuwa mwaminifu katika ndoa.Na jitahidi kuinua soka zaidi na zaidi, sasa umepata mke wako kabisa achana na wasichana.Salamu sana.Chibi.


Aksante mzee wa Sumo kwa picha na comments hizo.

No comments:

Post a Comment