Saturday, May 2, 2009

Idadi ya waliokufa Mbagala utata

IDADI ya watu waliopoteza maisha baada ya mabomu kulipuka katika ghala la kuhifadhia silaha la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni utata, ila si chini ya 18.
Magazeti ya leo yametoa idadi tofauti, kuna wanaosema ni 18, wengine wanasema 19, na wengine 20.
Hospitali ya Temeke jana ilithibitisha kupokea maiti 13 waliotokana na milipuko hiyo, miili tisa ni ya watoto iliyookotwa katika mto Kizinga eneo la Mbagala.
Kwa mujibu wa JWTZ askari sita walikufa katika milipuko hiyo ya mabomu iliyounguza ghala la silaha.
Rais Jakaya Kikwete amesema, ghala hilo halikujengwa katika makazi ya watu, kwa kuwa lilijengwa mwaka 1976 nje ya makazi hayo.

1 comment:

  1. hiyo nchi niya viongozi wazembe mara ya kwanza ilisha tokea kwani walikuwa hawakupata ufumbuzi wa kuhifadhi hayo mabomu nini wananafanya viongozi wanatakiwa kujiuzulu kama wenzao wa ulaya wanavyo fanya sio kungangania kwenye cheo for nothing kwa kujijenga wewe na family zao tujaribu kuchenji kitabia wananchi wapewe u free wa kuzungumza, hamna kuogopa viongozi ata awe raisi yeye ni binaadam kama sisi tuwe kama viongozi wa ulaya na serikari ya ulaya, wasinganganie vyeo kazi hawawezi, wanataka kujinufaisha wenyewe na family zao, kila mtu anataka good life,hawo wa kwanza hata hifazi hawajapata na wala msaada hawajapata sasa hii ni nini , sas na hii leo utawaeleza nini? ndugu rais? lazima viongozi wako wa chini wajiuzulu leo soon as possible ukiwa na wewe mwenyewe una mashaka

    ReplyDelete