Friday, April 10, 2009

Vyeti vinakodishwa!


Katibu Mtendaji wa NECTA, Joyce Ndalichako


KUNA mambo mengine ukiyasikia unaweza kudhani ni hadithi au simulizi za pwagu na pwaguzi kumbe ni kweli yametokea na pengine yanaendelea kutokea.

Uliwahi kufikiri au kutarajia kusikia kwamba mmiliki wa cheti halali cha kidato cha nne anaweza kukikodisha hadi kwa sh 400,000 kwa asiyenacho ili kitumike kuhalalisha utahiniwa wa muhusika?

Habari ndo hiyo, wanaousaka ualimu wanafanya hivyo, 61 kati ya hao wamepandishwa kizimbani kujibu tuuma za kughushi vyeti.

Vyuo vilivyohusika kwenye kashfa hiyo ni Montessori, St Francis Nkindo, Kange, Eckenford, Sahare, Bukoba Lutheran, Mpunguso cha Mbeya, Capital, Arafah, Chuo cha Ualimu Arusha, Greenbird, Tanzania College of Early Education na Salesian.

Watuhumiwa waliwasisha vyeti hivyo katika Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) ili wafanye mtihani wa ualimu daraja A na wa diploma ulioapangwa kufanyika Mei mwaka huu.

No comments:

Post a Comment