Wednesday, April 15, 2009

Unalea mtoto kumbe wa mwenzio!

MWANAUME jijini Dar es Salaam amejikuta katika wakati mgumu baada ya kubaini kuwa alikuwa anamlea mtoto asiye wake mwenye umri wa miaka minne.

Mke wa mwanaume huyo alimzaa mtoto huyo wakati wakiishi pamoja na aliamini kuwa ni mwanae. Wameishi pamoja kwa miaka tisa.

Jumapili iliyopita, siku ya Pasaka siri ilifikichuka, alibaini kuwa mtoto huyo (jina nilalo) si wake, ni wa mwanaume mwingine anayesadikiwa kuwa pia anaishi Dar es Salaam.

Siri hiyo ilifichuka baada ya baba mzazi wa mtoto huyo kutuma ujumbe mfupi kwenye simu ya mama wa mtoto huyo, akasahau kuifuta, mumewe akaikuta SMS hiyo kwenye simu ya mamsap wake.

Mke wa mwanaume huyo alihifadhi (alisave) jina la baba wa mtoto huyo kwenye simu yake kwa jina Mummy. Mwanaume huyo alipata hasira, akatishia kutanya 'kitu kibaya', mama mwenye nyumba akamsihi, akaacha.

Taarifa zilizopo ni kwamba, mama wa mtoto huyo amendoka kwa mwanaume huyo.

No comments:

Post a Comment