Wednesday, April 15, 2009

Mafuriko Moshi

KUNA habari kwamba wakazi kadhaa wa eneo la Mji Mwema kata ya Njoro, Moshi mkoani Kilimanjaro wamekumbwa na maafa baada ya maji kubomoa nyumba na kusomba mali zao usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mvua kubwa ilinyesha, mto unaopita jirani nao umefurika, maji yaliingia kwenye nyumba zao, baadhi zimebomoka, nyingine zimenusurika lakini maji yamejaa ndani.

1 comment:

  1. Kule njoro kuna nyumba ambazo misingi yake siyo imara, sijui kama zilishakarabatiwa na kila yanapotokea mafuriko, Njoro ndiyo huathirika kuliko maeneo mengine kwa sababu ya kuwa ukanda wa chini.
    Asante kwa taarifa, pengine tutaona picha baadaye.

    ReplyDelete