Thursday, April 9, 2009

Uchaguzi TLP utaisha salama?


Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa

OFISI ya Msajili wa vyama vya siasa imesema uongozi uliopo madarakani wa chama cha Tanzania Labour(TLP) ni halali na imekubali marekebisho ya katiba yaliyofanywa na Halmashauri kuu ya chama hicho.

Tamko hilo ni pigo kwa waliochukua fomu kushindana na Augustine Mrema katika uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Aprili 19 mwaka huu.

Hivi karibuni, mmoja wa wagombea hao aliandika barua kwa msajili akiiomba ofisi hiyo iunde kamati maalum kuandaa na kusimamia uchaguzi huo kwa madai kuwa uongozi wa Mrema hauna mamlaka hayo kwa kuwa ulimaliza muda wake Januari 30 mwaka huu.

Ofisi ya Msajili imekiri kuwa Mrema na wenzake walimaliza muda wake katika tarehe hiyo lakini imekubali kuwaongezea muda hadi Aprili 30 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment