SERIKALI imesitisha kazi ya kutafuta miili ya wachimbaji wadogo wa madini waliofukiwa katika machimbo ya Mgusu wilayani Geita, Mwanza kwa kuwa kwa hali ilivyo hakuna uwezekano wa kuendea na kazi hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda tangu jana yupo kwenye eneo la maafa, leo aliongoza kazi ya kuzika miili iliyopatikana.
Muda mfupi uliopita , Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, James Msekela amesema hadi sasa miili sita bado ipo chini hivyo kwa uamuzi huo, marehemu hao watahesabika kuwa wamezikwa humo.
No comments:
Post a Comment