Saturday, April 11, 2009

Kesho Pasaka, kumbukumbu ya Sokoine





WATANZANIA kesho wanaungana na wakristu wengine duniani kusheherekea kumbukumbu ya ufufuko wa Yesu Kristu.

Si hivyo tu, kesho ni kumbukumbu ya miaka 25 tangu Waziri Mkuu, Edward Sokoine afe katika ajali ya gari mkoani Morogoro Aprili 12 mwaka 1984.
Sokoine alikufa papo hapo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kugongwa na gari la mpigania uhuru wa Afrika Kusini, Dumisani Dube, Dakawa nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Binti wa Sokoine, Namelo amekaririwa akisema kuwa, shughuli maalum ya kumkumbuka baba yake itafanyika Agosti Modi Monduli Juu, Arusha.

No comments:

Post a Comment