WATOTO wawili wenye umri wa miaka tisa na saba wamefunga ndoa ikiwa ni kutimiza dhamira ya binti anayesubiri kuaga dunia nchini Marekani.
Watoto hao, Jayla Cooper(9) na Jose Griggs(7) walifunga ndoa takatifu Februari 22 mwaka huu ili kutimiza ndoto ya binti huyo aliye katika siku za mwisho za uhai wake kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu.
Watoto hao, Jayla Cooper(9) na Jose Griggs(7) walifunga ndoa takatifu Februari 22 mwaka huu ili kutimiza ndoto ya binti huyo aliye katika siku za mwisho za uhai wake kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu.
Wazazi wa watoto hao waliridhia watoto hao wafunge pingu za maisha, waliwasindikiza madhabahuni, na wakawapeleka hotelini kwa ajili ya honey moon.
Watoto hao wanaoishi Texas Marekani sasa ni mke na mume, wote wana kansa ya damu, lakini kwa mujibu wa maelezo ya daktari, safari ya Jayla duniani imefika ukingoni na kuanzia sasa wakati wowote ataaga dunia.
Jayla aligundulika kuwa ana saratani ya damu wakati akiwa na umri wa miaka 7 na moja ya ndoto katika maisha yake ni kuolewa, ameitimiza.
Alikutana na Jose wakati alipokaa kwa miaka miwili katika kituo cha afya cha watoto wanaosumbuliwa na saratani na matatizo mengine ya damu kilichopo Dallas, Texas.
Jose anaendelea vizuri, ana wakati mgumu kukubali ukweli kwamba mkewe Jayla hana siku nyingi za kuishi na kwa kuwa anampenda sana, hataki kuona ' anaenda'.
ebwana inasikitisha sana just imagen ungekuwe wewe ingekuwa vp? mungu awatangulie
ReplyDeleteeshima nautukufu tumrudishie bwana.
ReplyDelete