Saturday, April 4, 2009

Buriani Jade Goody


Jeneza lenye mwili wa Jade likipitishwa katika mitaa ya jiji la London


Mama mzazi wa Jade, Jackiey, akibembelezwa baada ya kuona jeneza lenye mwili wa mwanae





Eneo la makaburi la kanisa la Mtakatifu John atakapozikwa Jade



Jeneza lenye mwili wa Jade








Safari ya mwisho ya Jade

Jade wakati anaumwa

Mzazi mwenzie na Jade, Jeff akiwa na watoto wao



Jade na mumewe, Jack Tweed



Jade akirudi hospitali baada ya kufunga ndoa

MAMILIONI ya watu kote duniani wanashuhudia mazishi ya mtangazaji nyota wa vipindi halisi vya televisheni, Jade Goody(27).
Jade aliandaa mipango ya mazishi yake ikiwa ni pamoja kuchangua aina ya jeneza, eneo la kuzikwa, na kuagiza kuwa mazishi yake yawe ni sherehe kubwa kwa kuwa alifahamu kwamba watu wengi wangependa kumuaga.
Msafara wa mazishi yake una magari 21, umepita katika mitaa mbalimbali ya London, maelfu ya watu wamejipanga barabarani kumuaga, televisheni mbalimbali zinaonyesha LIVE.

Jade alifariki dunia Machi 22 mwaka huu, kutokana na ugonjwa wa saratani ya mfuko wa kizazi.

Agosti mwaka jana madaktari waligundua kuwa alikuwa na ugonjwa huo lakini tayari ulikuwa umesambaa kwenye sehemu nyingine za mwili akaelezwa kuwa hakuwa na siku nyingi za kuishi.

Nyota huyo wa shindano la Big Brother Uingereza alihakikisha anatimiza miongoni mwa ndoto kuu za maisha yake, KUOLEWA.

Huku akitambua kuwa alikuwa na wiki chache za kuendelea kuishi, Februari 22 mwaka huu alifunga ndoa na Jack Tweed(21), walilala pamoja usiku mmoja tu, na wakawa mume na mke kwa mwezi mmoja.

Jade ameacha watoto wawili, Bobby(5) na Freddie(4), aliozaa na mtangazaji wa kipindi cha X Factor, Jeff Braizer.
Watoto wa Jade hawatahudhuria mazishi yake, wapo Australia na baba yao.

No comments:

Post a Comment