HABARI tulizozipata hivi punde zimeeleza kuwa Mahakama Kuu Tanzania leo imewaachia huru watu watatu kati ya 13 waliokuwa wakituhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu na dereva wa teksi Januari 14, 2006, Dar es Salaam.
Jaji wa mahakama hiyo, Salum Massati amesema, ushahidi uliotolewa katika kesi hiyo hauonyeshi kama watu walihusika katika mauaji hayo kwenye msitu wa Pande, Dar es Salaam hivyo hawana kesi ya kujibu.
Mshitakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2006, Abdallah Zombe na wenzake tisa mambo bado ni magumu kwa kuwa mahakama imeona wana kesi ya kujibu.Hivi karibuni vyombo vya habari vilimkariri Zombe akisema kuwa hana kesi ya kujibu hivyo ataachiwa huru.
Jumla ya mashahidi 37 wametoa ushahidi katika kesi hiyo yenye mvuto nchini, na pia vielelezo 23 vimewasilishwa mahakamani.
Leo watu walifurika katika jengo la Mahakama Kuu Tanzania iliyopo barabara ya Magogoni, Dar es Salaam, na baada ya watu hao watayu kuachiwa huryu, ndugu, jamaa na marafiki waliwapokea huku wengine wakibubujikwa machozi, na wengine walilia kwa furaha.
Zombe na wenzake wapo rumande tangu mwaka 2006, na kuna uwezekano wa kuongezeka mashahidi wakiwamo viongozi wa polisi katika maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment