
KILA mtu anaweza kueleza maana ya mapenzi kwa namna anavyoweza lakini naamini moja ya vigezo atakavyotumia ni kwa namna gani mtu anavyoweza kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya mpenzi wake.
Tunaweza kufanya mengi kwa ajili ya wapenzi wetu lakini katika mazingira ya kawadia ya kibinadamu ni vigumu kuamua kufanyiwa operesheni ili kutoa sehemu ya viungo vyetu kuwapa tunaowapenda.
Mwanamke nchini Marekani amefanya hivyo, katoa figo yake moja kuokoa maisha ya mchumba wake, wanatarajia kufunga ndoa mwakani.
Mwanamke huyo, Elizabeth Kelly, ana umri wa miaka 28, amesema ametoa figo yake kwa kuwa Matthew House ni kila kitu kwake, duh!
No comments:
Post a Comment