Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania
Dkt.Jakaya Kikwete leo katika kilele cha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa
Amaan mjini Unguja.
Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amaan mjini Unguja.
Wananchi na maofisa wa Serikali wakiwa katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar leo
Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu alipowasili katika uwanja wa Amaan mjini Unguja wakati sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amaan.
Rais wa
Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika Uwanja wa Aman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwasalimu wananchi katika Uwanja wa Amani wakati wa sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
No comments:
Post a Comment