Thursday, November 19, 2015

Rais Magufuli ateua Waziri Mkuu



Rais Dk. John Magufuli amemteua Mbunge wa Ruangwa, Majaliwa Kassim Majaliwa (55) kuwa Waziri Mkuu.

Mwalimu Majaliwa amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Rufiji mkoani Pwani, Urambo mkoani Tabora, na amekuwa Mbunge tangu mwaka 2010. 

Awali, mwanasiasa huyo mwenye shahada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikuwa Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida.

Katika Serikali iliyopita, kiongozi huyo alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu.

Hadi sasa Majaliwa ni kocha wa Timu ya Bunge.

Wabunge wamempongeza Rais Magufuli kwa kumteua Majaliwa kwa maelezo kwamba, ni chaguo sahihi, ni mwadilifu, mchapakazi, ni mwaminifu, hana makundi, na ana uwezo wa kufanya uamuzi makini.


1 comment:

  1. You have done a great job. I will definitely dig it and personally recommend to my friends. I am confident they will be benefited from this site.

    ReplyDelete