Monday, July 27, 2015

Lowassa akaribishwa rasmi UKAWA

Wenyeviti wa vyama vinavyounda UKAWA wakizungumza na waandishi wa Habari leo.
Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

Zilikuwa tetesi, minong'ono na kama hadhithi tu, lakini sasa ni dhahiri kwamba, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amefanya uamuzi mgumu.


Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo umemkaribisha Lowassa kujiunga na umoja huo.

Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia amewaeleza waandishi wa Habari makao makuu ya Chama Cha Wananchi (CUF) Buguruni jijini Dares Salaam kuwa, Lowassa anakaribishwa katika umoja huo kwa kuwa ana uwezo mkubwa  wa kuhamasisha umma kuikataa CCM.

Mbatia amesema, Lowassa ni mchapakazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa kiutendaji katika majukumu anayokabidhiwa.

Alipoulizwa endapo Lowassa atagombea urais, Mbatia amesema, kila chama kina utaratibu wake hivyo mchakato ukishakamilika atatangazwa mgombea urais wa UKAWA.

Kwa mujibu wa Mbatia, mgombea huyo atatangazwa mwanzoni mwa Agosti mwaka huu.

No comments:

Post a Comment