Saturday, September 27, 2014

Nape awashambulia Chadema

 “Maandamano yenyewe yanayoruhusiwa na Katiba yana utaratibu wake na sheria za kufuata kabla ya kuandamana, lakini toka Chadema wameanzisha utaratibu wa maandamano wamefanikiwa kubadili nini zaidi ya kupoteza maisha ya watanzania wasiokuwa na hatia,”

“Lakini sasa tunajua siri ya maandamano yao, hali ya chama chao mbaya sana, kisiasa na kiuchumi. Katika kujaribu kutatua tatizo hilo wakabuni vurugu na fujo kupitia maandamano. 

“Picha za maandamano hayo watazipeleka nje ya nchi ili kuombea misaada ya pesa kwa kisingizio cha kupambana kujenga demokrasia kana kwamba nchini hakuna demokrasia na utawala bora,"


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

No comments:

Post a Comment