Thursday, September 18, 2014

'CCM mna madhambi, acheni fitina'

“Acheni, acheni dhambi ya kuwagawa na kuwasumbua watu. Punguzeni maneno na vijineno, CCM mnaongoza kwa vijineno, mnakoroga watu” 

 “Kazi yetu kutafuta uongozi, kupanga madiwani, mnakoroga watu, watu wanataka maendeleo, kuachana na umasikini, ninyi mnahangaika na vyeo, acheni kubeba watu,

“Hamuwezi mkaendelea wakati viongozi wanakoroga watu vichwa. Leo hadithi hii kesho hadithi hii, watu wanataka kujua umeme unakuja lini, meli inakuja lini, lakini ninyi ni vyeo, vyeo, vyeo tumewapa mnatusumbua,

CCM mna madhambi, mnakoroga watu, wanachama na viongozi wenzangu wa Chama cha Mapinduzi ndio wakorogaji wakubwa, halafu mtasingizia CUF, mtasingizi CHADEMA wakati mikorogo inaanzia kwenu,
 
“WanaCCM badilikeni, hawa wananchi wanataka maendeleo, wanataka kuondokana na umasikini. Wanaongoza nchi ni sisi, wanaoulizwa maswali ni sisi, lakini badala ya kushughulika na maendeleo yao, tumeishia kuvutana mguu huyu akisongea mbele huyu anamvuta mguu,
 
 “CCM mkitulia, Mafia itatulia, mnabaki CCM Nambari Wani, haiwi, itakuwa Nambari 10 kama mtaendekeza fitina zenu, kisiwa cha wananchi elfu arobaini kitapiga hatua kama mtashikamana na kuwa na umoja.”

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.

No comments:

Post a Comment