Friday, April 25, 2014

Walivyomuaga Mzee Cleopa Msuya


Rais Jakaya Kikwete akiwa viongozi wengine wakuu wa serikali chama cha Mapinduzi CCM, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana (kushoto) katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mara mbili katika awamu mbili tofauti, Mzee Cleopa David Msuya (wa kwanza kulia kwa Rais) ambaye amestaafu rasmi siasa baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 33.

Katibu wa CCM, wilaya ya Mwanga, akisoma historia fupi ya Mzee Msuya kabla na baada ya kujiunga na siasa

Mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM wilaya ya Mwanga, Joseph Thadayo akitoa salamu za marafiki na wasomi waishio nje ya Mwanga, ikiwemo salamu za Mwanasiasa maarufu na mdhamini wa CCM, Mzee Peter Kisumo ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na mzee Msuya katika Siasa.

Mzee Msuya akitoa pongezi zake kabla ya kuaga rasmi.

Rais Kikwete akizungumza na wananchi katika hafla ya kumuaga Mzee Msuya katika ulingo wa siasa, uliofanyika leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mwanga.





No comments:

Post a Comment